2013-12-14 11:50:40

Vijana wa Taizè kukutana kuanzia tarehe 28 Desemba hadi tarehe 1 Januari 2014


Jumuiya ya Kiekumene ya Taizè inaendelea kukamilisha maandalizi kwa ajili ya vijana kutoka sehemu mbali mbali za Ulaya, watakaokutanika mjini Strasburg, kuanzia tarehe 28 Desemba hadi tarehe Mosi, Januari 2014. Hiki kitakuwa ni kipindi cha vijana kushiriki mwaliko wa Jumuiya ya Kiekumene ya Taizè kwenda kujichotea utajiri wa Kiinjili unaofumbatwa katika: Sala, Tafakari ya Neno la Mungu na Ukimya.

Huu ni mwendelezo wa hija ya maisha ya kiroho miongoni mwa vijana iliyoanzishwa na na Frà Roger kwenye miaka 1970 na leo hii kuna maelfu ya vijana ambao wanashiriki katika mikutano hii ya maisha ya kiroho, inayowakutaanisha vijana kutoka katika dini na madhehebu mbali mbali ya Kikristo, kwa lengo la kusali na kutafakari pamoja Injili ya Furaha.

Itakumbukwa kwamba, kunako mwaka 2012, Vijana wa Taizè walikutana mjini Roma pamoja na kupata neno na tafakari kutoka kwa Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto XVI.







All the contents on this site are copyrighted ©.