13 Desemba ya mwaka 1969, miaka 44 iliyopita, historia ya maisha ya Jorge Mario
Bergoglio ilifunua ukurasa mpya, baada ya kula kiapo cha kujiunga katika daraja Takatifu
la Upadre, chini ya kanuni ya shirika la Kitawa la Wajesuiti.
Mkurugenzi wa
Idara ya Maadili ya kitauhidi, katika Chuo Kikuu cha Kipapa Gregorian, Padre Miguel
Yanez, Mjesuit , Mu-argentina, Mwenye kumfahamu Papa kwa ukaribu zaidi , katika kipindi
cha miaka ya nyuma, katika mahojiano na Radio Vatican , ameyaeleza maisha ya Padre
Bergoglio, kwamba, tangu kumfahamu , wakiwa nchini mwao, maisha yake ya Kipadre,
daima alipenda kushirikiana na wengine katika yote, iwe maisha ya kijumuiya na kikanisa
, Ibada za Misa,au kimasomo, na hata palipokuwa na nafasi za burudani, alishiriki
vyema. Hizi ni kumbukumbu zilizobaki kwa wengi.
Padre Yanez amesema, Padre
Begoglio tangu mwanzo alikuwa na mvuto kwa watu na alipenda kukutana na watu na kushirikishana
nao mengi yakiwemo matatizo, hasa hali ngumu za kutatiza. Daima aliwadumisha watu
katika kuwa na tumaini la kupata ufumbuzi kwa njia ya kushirikishana mawazo.
Na
akirejea kuchaguliwa kwa Papa Francisko na gazeti la Times Magazine kuwa mtu mashuhuri
wa mwaka, amesema , kuchaguliwa kwake kunatoa ujumbe, kwanza wa kumtakia mema, kwake
yeye Papa Francesco ambaye siku za nyuma alijaribu kila njia kuviepa vyombo vya habari,
maana alitenda si kwa kutafuta ufahali katika vyombo vya habari bali kw amoyo w aupndo
wa ndani katika kuhudumia wengine. Alifanya mengi kimyakimya kisiri bila kutafuta
makuu. Lakini kwa sasa amejikuta mbele ya vyombo hivyo na Huduma yake sasa si siri
tena, maana anatazamwa na dunia zima. Na Kanisa linahitaji mtu kama huyu, kuufikisha
ujumbe wa Injili kwa watu wote, kupitia njia zote. .