Papa : Wakristo wenye mzio na wahubiri daima ni wakosoaji, wenye kumfungia nje Roho
Mtakatifu
Wakristo wenye kuwa na mzio(allergic) na wahubiri daima huwa na jambo la kukosoa.
Lakini, katika hali halisi, ndani mwao wana woga fulani wa kumfungulia mlango Roho
Mtakatifu. Ni watu wenye kuwa na wasiwasi, mashaka na huzuni ndani mwao. Papa Francisko
alieleza wakati wa Ibada ya Misa, aliyo iongoza katika Kanisa dogo la Mtakatifu
Marta mapema asubuhi ya Ijumaa hii Vatican..
Homilia ya Papa ikilenga katika
somo la Injili ambamo Yesu analinganisha kizazi cha nyakati zake na watoto wanaowaita
wengine kucheza pamoja, lakini wanakataa kuitikia wito huo kwa sababu hawajui kucheza
na wengine kwa furaha, kwao hakuna lililo jema, ila wasiwasi na huzuni. Papa
amefafanua kwamba, watoto hao wanaokataa ni sawa na watu wasiopenda kujifunua kwa
neno la Mungu, ambao kwao si hukataa kusikiliza ujumbe wa Neno lakini humkataa mjumbe
mwenyewe, kama walivyo mkataa Yohane Mbatizaji, wakisema hali wala kucheza nao, wakimwita
ni mwenda wazimu. Na pia walimkataa Yesu wakimwita ni mlevi, rafiki wa watoza ushuru
na wenye dhambi. Watu hao daima, walikuwa na sababu za kumkosoa mhubiri.
Papa
amesema , Wakristo wa namna hii, wanasikitisha kwa sababu hawaaamini katika nguvu
ya Roho Mtakatifu, hawaamini katika uhuru unaopatikana katika kusikiliza mahubiri,
ambamo mna mafundisho na maonyo. na pia mna uhuru mwingi unaolipa kanisa nguvu za
kusonga mbele. Hawa ni Wakristu wenye kuwa hofu za kufurahi na wengine, hofu katika
kila jambo, hata usalama wao. Hili linasikitisha kwa sababu daima huwa na tabia ya
kukosoa wahubiri wa ukweli, kwa sababu wanaogopa kufungua mlango kwa Roho Mtakatifu.
Papa alisema, tuombe kwa ajili yao, na tuombe pia kwa ajili yetu, ili kwamba
pasiwe na Wakristo wa aina hii waliojaa huzuni,,wasiwasi na mashaka, wenye kukataa
kumfungulia mlango Roho Mtakatifu. Ili waruhusu Roho Mtakatifu kuingia kwa uhuru,na
kukaaa ndani mwao. Roho Mtakatifu anaye kuja kwetu kwa njia ya kashfa ya Mhubiri.