Katika Maadhimisho ya Jubilee ya Miaka 50 ya Uhuru wa Kenya, Serikali ya DRC pamoja
na Jeshi la M23, siku ya Alhamisi tarehe 12 Desemba 2013 wametiliana mkataba wa amani,
tukio ambalo limeshuhudiwa na viongozi mbali mbali wa Serikali waliokuwa wanahudhuria
Jubilee ya Miaka 50 ya Uhuru wa Kenya mjini Nairobi.
Taarifa hii imebainishwa
na Bwana Manoa Eisipisu, msemaji wa Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya. Ni matumaini ya
wananchi wengi wa DRC kwamba, mkataba huu uliotiwa sahihi na wadau husika hautafungiwa
kwenye makabati ofisini na watu wakaendelea kutwangana mitaani! Tukio hili limeshuhudiwa
na Rais Joyce Banda kutoka Malawi ambaye pia ni Mwenyekiti SADC pamoja na Rais Yoweri
Kaguta Museveni wa Uganda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Nchi za Maziwa Makuu.
Viongozi
watambue kwamba, wana dhamana ya kimaadili na kisheria kuhakikisha kwamba, wanatekeleza
makubaliano haya kwa ajili ya mafao na ustawi wa wananchi wa DRC ambao kwa miaka mingi
wameendelea kuteseka kutokana na vita pamoja na kinzani za kijamii na kisiasa.