2013-12-12 11:12:05

Hali bado ni tete Afrika ya Kati!


Wachunguzi wa masuala ya kivita wanasema, hali bado ni ngumu sana Jamhuri ya Watu wa Afrika ya Kati. Milio ya risasi na milipuko ya mabomu inaendelea kusikika, vitendo vinavyoendeshwa na Kikosi cha Seleka pamoja na wanajeshi ambao wameendelea kuwa waaminifu kwa Rais Francois Bozize aliyeng'olewa madarakani Mwezi Machi 2013.

Kinzani hizi za kivita zinakwamisha zoezi la kuwanyang'anya wanajeshi silaha, mchakato unaofanywa na vikosi vya kijeshi kutoka Ufaransa, vinavyofanya operesheni maalum mjini Bangui, ambako hivi karibuni watu mia nne walipoteza maisha yao kutokana na mapigano.







All the contents on this site are copyrighted ©.