Vatican, Ijumaa kuwasha rasmi, taa za mti wake wa Krismas
Taarifa imetolewa kwamba, taa za Mti wa Krismasi uliowekwa katika uwanja wa Kanisa
Kuu la Mtakatifu Petro, ambao ulitolewa huko Waldmünchenu Ujeruman, taa zilizopamba
mti huo, zitawashwa rasmi Ijumaa,13 Desemba, majira ya saa kumi na nusu za jioni.
Taarifa hiyo , kutoka Ubalozi wa Ujerumani katika Jimbo Takatifu, inasema,
hii ni mara ya kwanza tangu mwaka 1984, kwa mti wa Krismasi unaowekwa katika uwanja
wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, kutoka Ujerumani, kutoka mji wa Waldmünchenu wa
Upper Palatinate Ujerumani.
Kwa ajili ya tukio la kuwasha taa zilizopamba
mti huo, utakuwepo ujumbe mkubwa wa uwakilishi wa mkoa wa Waldmünchenu, ukiongozwa
na Askofu Rudolf Voderholzer wa Regensburg, akiwepo pia Rais wa kile kinachoitwa
Frenckfestspiele, bwana Franz Löffler na pia ujumbe kutoka Jamhuri ya Czech, Askofu
František Radkovský wa jimbo la Pilsen. Aidha serikali ya Bavaria itawakilishwa na
Waziri wa Mambo ya Ulaya na Mahusiano ya Mkoa , Dk Beate Merk . Na Serikali ya Shirikisho
la Ujeruman, itawakilishwa na Katibu wa Wizara ya Shirikisho kwa ajili ya ulinzi
utamaduni wa Mkristo, Mheshimiwa Schmidt.