2013-12-11 15:40:23

Mwaka mmoja umetimia tangu Twitter@pontifex kuzaliwa


Tarehe 12 Desemba, unatimia mwaka mmoja tangu Papa Benedikto XVI, alipojiunga katika mtandao wa mawasiliano jamii kwa kufungua ukurasa wake wake wa Twitter @ Pontifex , kama juhudi za kuitangaza Injili katika mitandao ya kijamii. Tukio hili la Kimataifa , linaendelezwa na Papa Franicisko.

Taairfa zinabaini kwamba, mpaka sasa, ukurasa huu unao toa ujumbe wa Papa katika lugha tisa mbalimbali za kimataifa, umetembelewa na watu wasiopungua millioni 11 toka pande mbalimbali za dunia.

Askofu Mkuu Claudio Maria Celli , Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Mawasiliano ya Jamii , akiuzungumzia ukurasa huu anasema, Papa Benedikto XVI, alizindua anwani yake katika twitter kwa mara ya kwanza, kwa kutambua kikamilifu umuhimu wake, hasa katika lugha na uwanja wa kukutana na vijana wengi zaidi. Na leo hii, lugha hii inayo endelezwa na Papa Francisko, kama takwimu zinavyojionyesha, imekuwa na mwelekeo chanya, wa kutoa tone la maji ya uzima , katika roho iliyokaukiwa na neno. Na imeonekana kuwa ni njia nzuri ya kusambaza neno la Yesu, hasa kwa wale ambao hawana mahali pengine pa kuupata ujumbe wa Yesu.

Askofu Mkuu Celli anadhani kwamba, hii ni changamoto kwa waamini wote, kubuni njia mpya za kufikisha ujumbe wa Injili katika mazingira ya sasa, na kuondokana na fikira kwamba uinjilishaji mpya ni kazi ya wamisionari. Katika mazingira ya " digital ", ni lazima kuhakikisha kwamba neno la Injili linasikika pia humo.

Askofu Mkuu amefanya rejea kwa maneno ya Benedict XVI, aliposema kuwa, si tu kutoa ndondoo rasmi za Injili katika mtandao, lakini katika mazingira haya , ni lazima kutoa tathmini za maisha na ushuhuda binafsi. Na amesisitiza katika mtazamo huu, kwa wafuasi wa Bwana , lazima imani yao ionekane wazi katika utendaji wa kila siku .

Na kwamba, kama Papa Francisko alivyosema katika waraka wake wa Injili ya Furaha, changamoto kubwa kwetu leo hii ni kutangaza injili katika lugha inayoeleweka kwa ufasaha zaidi . Na ameonya dhidi ya hatari ya lugha inayo weza kubadilisha maana ya ujumbe wa Injili. Na hivyo alitaja haja ya kutumia lugha ambayo watu leo wataelewa kwa urahisi zaidi.








All the contents on this site are copyrighted ©.