Mlango wa Bwana daima ni wazi na kutupatia tumaini.
Hatupaswi kuhofia ukombozi wa Bwana , badala yake , ni kujiweka tayari kwa ajili ya
ujio wake. Ni kuufungua mlango wa moyo na kumpokea kwa matumaini. Papa alieleza katika
homilia yake wakati wa Ibada ya Misa, mapema asubuhi Jumanne, katika Kanisa dogo
la Mtaktifu Marta hapa Vatican.
Papa alitafakari maneno ya somo la kwanza,
kutoka Kitabu cha Nabii Isaya, ambamo Nabii Isaya anasema, "farijikeni enyi watu
wangu, Bwana, yu karibu na watu wake, kuwatuliza ,na kuwapa amani". Papa ameeleza
kazi hii ya kufariji, ina uwezo wa kubadili yote. Bwana, kweli ana uwezo wa kuviumba
vyote upya .
Bwana hufanya vyote kuwa vipya . Na kanisa Kamwe halichoki kutangaza
habari hii ya uwezo wake wenye nguvu ya kufanya vitu vyote upya ,na huvifanya katika
maajabu yake. Na kwa namna hiyo , huwatembelea watu wake, akiwafanya kuwa viumbe
wapya, kwa uwezo wake Mkuu. Papa alieleza kwa kurejea pia maneno ya mwisho ya Yusuf
kwa ndugu zake , kwamba , Bwana atawatembelea. Na wakati Bwana atakapo watembelea,
wachukue pia mifupa yake pamoja nao. Bwana kutembelea watu wake, lilikuwa ni tumaini
la Israeli. Na aliwatembelea na kuwafariji.
Akiendelea kufafanua maana kutembelea
na kufariji , alisema, Bwana hufanya hivyo mara nyingi tu, hata kwetu pia, katika
ulimwengu huu wetu. Papa alisisitiza mambo mawili, kwamba, Wakati Bwana atakapokuja
atatupa tumaini ,ambalo ni lina uwezo wa kweli katika maisha yote ya Kikristu. Hii
ni neema,na ni zawadi.
Na akaonya kwamba, pale Mkristu anaposahau tumaini
hili, au mbaya zaidi kupoteza matumaini, maisha yake pia hupoteza maana. Lakini
Bwana hachoki kuwapokea wanao mrejea , na huwafariji na kuwapa tumaini jipya. Na hufanya
hivyo kwa upole mkuu na huwa karibu na kila mmoja wetu , kwa sabab u yeye huwafariji
wake wake na humfariji kila mmoja wetu. Yeye ni Mchungaji mwema mwenye kulichunga
kundi lake la kondoo, kw amkono wake huwakusanya wanakondoo na kuwapeleka kaika malisho
yake mazuri na kuwahudumia kwa wema wote..
Papa alieleza na kumalizia kwa
kutazama jinsi Yesu alivyoishi na wafuasi wake , Maria Magdalene na wale wanafunzi
wa Emmaus . Pia kwa Tomas aliyemwambia weka kidole chako hapa. Hivyo ndivyo Bwana
alivyowafariji na kuwapa tumaini wanafunzi wake. Papa alisali ili Bwana atupatie sisi
sote neema ya kutoogopa kufarijiwa na Bwana , bali kuwa tayari kufungua mlango wa
moyo na kumwomba neema hii ya matumaini na kuwezeshwa kuusikia wema wa Mungu Baba.