2013-12-10 09:39:42

Papa Francis anakutana na Rais wa Jamhuri ya Kongo, Denis Sassou N'guesso


Jumatatu 09.12. 2013, Papa Francisko alikutana na Rais wa Jamhuri ya Congo , Mheshimiwa Denis Sassou N'guesso .
Taarifa iliyotolewa na Vatican inasema, Baba Mtakatifu Francisko na mgeni wake , walizungumzia zaidi mchango wa Kanisa Katoliki kwa watu wa Congo, hasa katika nyanja ya afya na elimu. Na pia waligusia uhusiano kati ya Jimbo Takatifu na Jamhuri ya Congo na kuahidi kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizi mbili.
Na mwisho, walibadilishana mawazo juu ya hali ya kisiasa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati ambapo waasi Kiislamu wa Seleka, wanaendesha kampeni ya ugaidi dhidi ya raia na dhidi ya makanisa ya Kikristo. Walikubaliana kwamba kuna haja ya kuwa makini hasa katika utoaji wa huduma kwa wakimbizi na watu walio timuliwa makwao , na kushughulikia kwa kina zaidi , tatizo la ukosefu wa usalama katika kanda hiyo ikiwa ni pamoja na kukua kwa wimbi la ubabe wa kupindukia.







All the contents on this site are copyrighted ©.