2013-12-09 10:08:44

Tata Madiba kuzikwa na wakuu wa nchi 53


Wakuu wa nchi 53 wanatarajiwa kuhudhuria katika mazishi ya Mzee Nelson Mandela, aliyefariki dunia hapo tarehe 5 Desemba 2013, mjini Johanesburg, Afrika ya Kusini. Wananchi watapata fursa ya kutoa heshima zao za mwisho kwa Tata Madiba, Jumanne, tarehe 10 Desemba, 2013, kwenye Uwanja wa Michezo wa Johanesburg.

Kuanzia tarehe 11 Desemba 2013 hadi tarehe 13 Desemba 2013, Mwili wa Tata Madiba utawekwa kwenye Jengo la Serikali, Pretoria, Afrika ya Kusini na Jumapili, tarehe 15 Desemba, 2013, Mzee Nelson Mandela atazikwa Kijijini kwake Qunu, alikozaliwa na kukulia.









All the contents on this site are copyrighted ©.