Maria Mkingiwa dhambi ya Asili ni tunda la Upendo wa Mungu- Papa
Maria kutungwa mimba bila dhambi ya asili, ilivyo andikwa katika mpango wa Mungu,
ni tunda la upendo wa Mungu, kuikomboa dunia dhidi ya dhambi, Baba Mtakatifu Francisiko
alieleza wakati wa sala ya Malaika wa Bwana , siku ya Jumapili, mbele ya mahujaji
na wageni waliokusanyika katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro. Hotuba fupi
ya Papa ililenga katika Siku Kuu ya Maria Mkingwa dhambi ya Asili, ambayo pia ilikuwa
ni Jumapili ya Pili ya Kipindi cha Majilio.
Papa aliendelea kuitafakari sherehe
ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya Asili, akisema, katika Siku kuu hii, macho yetu
tunayaelekeza katika uzuri wa Mama wa Yesu , Mama Yetu, na kwa furaha kubwa , Kanisa
linatafakari maneno ya Mtakatifu Luka “ amejaa neema" kama ilivyoandikwa katika Injili
ya Luka ( Lk 1:28). Bikira Maria Mama yetu, zaidi ya yote, anatuongoza sisi katika
mwendo wetu tunapoelekea kuisherehekea Siku Kuu ya kuzaliwa mwanae Yesu Kristu,
Siku Kuu ya Noel. Maria Mkingiwa dhambi ya asilia, anatufundisha jinsi ya kuishi wakati
huu wa kusubiri ujio wa Bwana.
Papa alifafanua zaidi kwamba, Maria kukingiwa
dhambi ya asili tangu wakati wa kutungwa mimba , iliandikwa katika mpango wa Mungu,
na ni tunda la upendo wa Mungu, katika kumkomboa binadamu dhidi ya dhambi.
Baada
ya kuongoza sala ya Malaika wa Bwana , Papa alionyesha ukaribu wake kwa Kanisa Amerika
Kaskazini,ambako lilikuwa likisherehekea miaka 350 ya Parokia yake ya kwanza ya Mama
Yetu wa Quebec “Notre- Dame de Québec”.Na ahitimisha kwa kuwatakia wote, Siku Kuu
njema ya Mama Yetu Mkingiwa dhambi ya Asili.