2013-12-09 09:43:40

Kardinali Peter Turkson , kumwakilisha Papa katika mazishi ya Mandela


Baba Mtakatifu Francisko , amemteua Kardinali Peter Turkson, Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Haki na Amani , kuwa mwakilishi wake maalum, wakati wa Maziko ya Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela.
Nelson Mandela alifariki Alhamisi ya wiki iliyopita akiwa na umri wa miaka 95, kwa maradhi ya mapafu. Mwana huyo maarufu wa Afrika. Jumanne tarehe 10 Desemba 2013, watu watapata nafasi ya kutoa heshima zao za mwisho na maziko ni hapo jumapili tarehe 15 Desemba 2013.








All the contents on this site are copyrighted ©.