Afrika Kusini na dunia kwa ujumla iko katika maombolezo ya kuondokewa na mtu mashuhuri
duniani,Nelson Madiba Mandela, Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, na mshindi wa Tuzo ya
Amani, ambaye amefariki dunia kwa homa ya mapafu. Nelson Madiba Mandela alifariki
usiku wa Alhamis kuamkia Ijumaa, akiwa na umri wa miaka 95 na alikuwa na umri wa miaka
95.
Nelson Madiba Mandela, dunia inamkumbuka kama mfano wa mtu wa amani,
msahemevu na shujaa, aliye aliongoza Afrika Kusini kutoka mikononi mwa watawala wachache
wabaguzi wa rangi, baada ya kufungwa jela kwa miaka 27. Pia anaheshimiwa kuwa nembo
ya kiongozi adilifu duniani.
Rais Jacob Zuma, alitangaza habari za kifo cha
Mandela Alhamisi usiku kwenye televisheni, akisema Nelson Mandela aliyejulikana kwa
jina la ukoo , Madiba, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 95, majira ya 20:50,
Desemba 05, 2013 akiwa nyumbani kwake, karibu na familia yake.
Rais Zuma amesema,
Yeye sasa kapumzika. Yeye sasa yuko katika amani ya kudumu. Afrika Kusini imepoteza
mwana wake mkuu, na Baba wa taifa. ' Mara baada ya habari za kifo cha Nelson
Mandela, kutangazwa , nchini Afrika Kusini , wakazi wa kitongoji cha Soweto, ambako
kuna weusi wengi, walikusanyika katika mtaa wa karibu na nyumba ambapo yeye Nelson
Mandela aliwahi kuishi. Waliimba na kucheza kwa kuomboleza kifo chake, kama ilivyo
mila na desturi za utamaduni wao.
Kwa heshima yake , bendera zote za kitaifa,
zinapeperuka nusu mlingoti mpaka baada ya mazishi, ambayo tarehe bado kutajwa. .
Na habari tokea mtaa wa Houghton kitongoji cha Johannesburg ambako kuna nyumba yake,
watu walikusanyika, wakiwa na simanzi za kusisimua , ambako baadhi waliimba nyimbo
za maombelezo , na wengine walipiga mbiu ya vuvuzela, na picha zenye sura ya Mandela
akitabasamu zilizotundikwa juu ya miti kukiwa na maneno Madiba pumzika kwa amani,
Pia watu wametengeneza kaburi la bandia ambako wameweka mishumaa , bendera za taifa
na mashada ya maua.
Historia ya Nelson Madiba Mandela : 1918
Alizaliwa katika mkoa wa Eastern Cape , katika familia , kitemi. Mandela alikulia
kijijini, ambako alipata mafunzo mazuri ya kuwa kiongozi, na baba yake alifariki
na kumuacha katika umri wa miaka tisa. Mandela katika maisha yake alisifu malezi aliyoyapata
kutoka kwa baba yake ambaye alipenda utu wema na uadilifu katika maisha. Nelson
Mandela alikuwa muumini wa kanisa la Methodist, alisoma katika shule ya Kimethodist
na alipita katika vyuo vikuu mbalimbali , Chuo Kikuu cha Fort Hare, Chuo Kikuu cha
London, Chuo Kikuu cha Afrika Kusinina Chuo Kikuu cha Witwatersrand.
Mwaka
1943 akajiunga na chama cha ANC . Na kwamba ndoa zake mbili za kwanza zilivunjika
kutokana na yeye kuchukua muda mwingi zaidi katika masuala ya kisiasa.
Alifunga
ndoa na Mke wake wa Kwanza Evelyn Wase, 1944 na walizaa watoto watatu na waliishi
maisha mazuri. Lakini mwaka 1954 wakati Mandela alipokamatwa kwa makosa ya uhaini
kwa mara ya kwanza , na kuwekwa jela na baadaye kutolewa baada ya kuwekewa dhamana
, Mandela alimkuta mkewe kaondoka na kuacha watoto wao wadogo wawili. Everlyn alirudi
kwao na baadaye kuolewa na mwanaume mwingine.
Baadaye, katika harakati za
kisiasa, Mandela alikutana na Winnie Madikizela , wakati alipokamatwa mara ya pili
kwa kesi ya uhaini na kufungwa kwa miaka miwili. Kunako mwaka 1958 walifunga ndoa
na Winnie Madikizela na walizaa watoto wawili wa kike, kabla Mandela hajafungwa gerezani
mwaka 1964. Na baada ya kuhukumiwa kifongo cha maisha,maisha yao kama mke na mme yaliendelea
kwa njia ya barua na Winnie kumtembelea gerezani,hadi Mandela alipoachiwa huru mwaka
1990, Winnie alimchukua Mandela kama mme , lakini kumbe wakati huohuo, kifichoni alikuwa
na bwana mwingine kijana zaidi. Na mwaka 1992, walitangaza kutengana rasmi.
Na
mke wa tatu, Graca Machel, alianza kufahamiana na Nelson Mandela mwaka 1986 baada
ya kifo cha mmewe Samora Michel. Mwaka 1996 , Nelson na Graca walifungishwa ndoa na
Rais Robert Mugabe, ambaye ameishi nae muda wote hadi kifo chake, lakini hakuzaa nae
mtoto.
Watoto wa Nelson Madiba Mandela ni Madiba Thembekile Mandela. Makaziwe
Mandela, , . Zenani Mandela, Zindziswa Mandela.
Maisha ya kisiasa
kwa ufupi yanataja : Alijiunga na ANC mwaka 1943. 1956 Alifunguliwa
kesi ya uhaini lakini baada ya miaka minne kiasi ikafutwa. 1962 Alikamatwa na
kushitakiwa kwa kosa la uchochezi na kufungwa jela miaka mitano. 1964 Alishitakiwa
kwa kosa la kuhujumu serikali na kupewa hukumu ya kifungo cha maisha. 1990 Aliachiliwa
huru kutoka gerezani, na 1993 alitajwa kuwa mshindi wa tuzo heshima ya Amani.
1994 alichaguliwa Rais wa kwanza mweusi Afrika Kusini. 1999, aliachia
madaraka hayo. 2001 Aligunduliwa kua na Saratani ya tezi kibofu 2004 alitangaza
kustaafu maisha ya kisiasa. 2013 Desemba 5, amefariki dunia