Nelson Madiba Mandela mfano wa kiongozi bora- Obama
Viongozi mbalimbali wa dunia wanapeleka salaam zao za rambirambi kwa familia ya Nelson
Mandela na raia wote wa Afrika Kusini kufuatia kifo cha Nelson Madiba Mandela. Rais
Barack Obama, wa Marekani katika salam zake za rambirambi, ameikumbuka historia
ya Nelson Madiba Mandela na kueleza kuwa yeye Obama ni kati ya mamilioni ya watu waliovutiwa
sana na ushujaa wa Nelson Madiba.
Obama ametaja machache yaliyomvuitia toka
kwa Madiba kuwa ni pamoja na maneno aliyo yatoa wakati wa kesi yake mwaka 1964, ambako
akiwa kizimbani alisema, ' Nimepigana kwa bidii dhidi ya udhalimu wa utawala wa wazungu
wachache, na pia dhidi ya utawala wa weusi wachache.
'Mimi ninapendelea
jamii yenye demokrasia, jamii huru, ambamo watu wote wanaishi kwa amani na fursa
sawa. Ni mawazo ninayotumiani kuyaishi na kuyafanikisha , hata kama italazimu kifo
kwa ajili hiyo. Rais Obama anasema, kweli Nelson Mandela aliishi kwa lengo hilo ,
na alilifanikisha na leo hii ametutoka kwa amani. Ni lengo linalotakiwa kufanikishwa
na kila binadamu.
Na kwamba, dunia imempoteza moja wa watu mashuhuri, jasiri,
mwama na diliafu, anayefaa kuigwa na binadamu wote, katika maisha ya hapa duniani.
Yeye daima atakuwa mfano wa maisha bora. Na kupitia heshima na unyenyekevu na mapenzi
yake thabiti katika kujitolea sadaka kwa ajili ya uhuru wake mwenyewe na uhuru wa
watu wengine, Madiba kwa kushirikiana na wengine aliibadili Afrika Kusini.
Rais
Barack Obama ameomba , safari ya Madiba tangu kuwa mfungwa gerezani hadi Urais, na
iangaze na kutoa uvuvio kwa kila binadamu katika kubadili ubaya na kuwa wema na katika
kudumisha ahadi ya kusamehe, amani na mapatano, si nchini mwake tu lakini katika
mataifa yote na hata katika maisha yetu binafsi.Huo ndiyo urithi mkuu ulioachwa na
Madiba kwa dunia yote.