2013-12-06 15:59:31

Mzee Madiba kuzikwa Kijijini kwake hapo tarehe 15 Desemba 2013


Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini ametangaza kwamba, Mzee Nelson Mandela atazikwa kwa heshima zote za kitaifa Jumapili tarehe 15 Desemba 2013, Kijijini kwake Qunu na kwamba, wananchi wa Afrika ya Kusini na nchi jirani watapata nafasi ya kutoa heshima zao za mwisho kwenye Uwanja wa michezo ulioko mjini Johanesburg hapo tarehe 10 Desemba 2013.

Kuanzia tarehe 11 Desemba 2013 hadi wakati wa mazishi, mwili wa Marehemu Mzee madiba utakuwa kwenye majengo ya Serikali mjini Pretoria. Jumapili tarehe 8 Desemba, 2013 ni Siku ya Maombolezo kitaifa; wakati wa sala na tafakari ya kina kuhusu mchango wa Mzee Madiba katika maisha na ustawi wa wananchi wa Afrika ya Kusini na Ulimwengu katika ujumla wake. Mashirika ya ndege nchini Afrika ya Kusini yameonesha utayari wa kuwasafirisha waombolezaji hadi kwenye matukio maalum.







All the contents on this site are copyrighted ©.