2013-12-06 12:23:14

Askofu msaidizi Monfort Stima ateuliwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Mangochi, Malawi


Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 6 Desemba 2013 amekubali ombi la kung'atuka kutoka madarakani lililotolewa na Askofu Alessandro Pagani, S.M.M. kadiri ya sheria za Kanisa namba 401ยง 1. Baba Mtakatifu ameteua Askofu msaidizi Monfort Stima wa Jimbo kuu la Blantyre, kuwa Askofu mpya wa Jimbo la Mangochi, nchini Malawi.







All the contents on this site are copyrighted ©.