2013-12-03 12:10:15

Mwanamuziki Tabu Ley, aaga dunia


Tabu Ley Rochereau, mwanamuziki maarufu na mwanzilishi wa mtindo wa rumba wa soukous,akijulikana kama"Mfalme wa Rumba la Congo" ambaye alikuwa mmoja wa wanamuziki waliopendwa barani Afrika, amefariki dunia, Jumamosi katika hospitali moja mjini Brussels, Ubelgiji, kwa maradhi ya kiharusi. .
BBC, imetaarifu kwamba Tabu Ley Rochereau, Mwanamuziki huyo akiitwa Pascal-Emmanuel Sinamoyi Tabu alizaliwa wakati wa utawala wa Wabelgiji nchini Congo mwaka 1937 au 1940, kutegemea na vyanzo vya habari, alikuwa akiumwa tangu mwaka 2008 akisumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi.
Mwana muziki , Tabu Ley Rochereau , Kiongozi wa bendi ya Orchestre Afrisa International alikuwa ni kiongozi mbunifu ambaye uimbaji wake uliunganisha sauti za muziki wa Kiafrika, Cuba,na mirindimo ya Caribbean, na aliimba bila kuchoka na kubandikwa jina la "Sauti ya Mwangaza."
Muziki wa Tabu Ley unapatikana katika mamia ya santuri za LP. Miongoni mwa santuri hizo ni ile ya Ley, Ley, Seigneur Ley Rochereau. Pia kwa weledi mkubwa kazi zake zimekusanywa katika CD.
Miongoni mwa miziki iliyo mpa umaarufu mkubwa Tabu Ley ni Muzina, Maze, C'est comme ca la vie, selikutu, Ibeba, Nadina na nyingine nyingi.








All the contents on this site are copyrighted ©.