2013-12-03 08:35:26

Mshikamano wa dhati na watu waliokumbwa na ajali ya Helkopta Uingereza!


Baba Mtakatifu Francisko ametuma salam za rambi rambi kwa wote walioguswa na ajali ya Helkopta iliyotokea mjini Glasgow, Uingereza mwishoni wa juma na hivyo kusababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao. Baba Mtakatifu anapenda kuwafariji wote kwa njia ya uwepo wake wa sala na sadaka takatifu, wakati huu wa maombolezo na majonzi makubwa.

Ujumbe wa Baba Mtakatifu umeandikwa kwa niaba yake na Askofu mkuu Antonio Mennin, kwenda kwa Askofu mkuu Philip Tartaglia wa Jimbo kuu la Glasgow, Uingereza.

Hadi kufikia siku ya Jumatatu, watu tisa tayari walikuwa wamekwisha poteza maisha, pengine idadi hii inaweza kuongezeka.







All the contents on this site are copyrighted ©.