Jengeni urafiki na Yesu, ili awaonjeshe upendo wa dhati!
Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii anawakumbusha
kwamba, wote wanaalikwa kujenga na kudumisha urafiki na Yesu. Anawataka wasiwe na
wasi wasi wa kujiachilia mikononi mwa Yesu ili aweze kuwaonjesha upendo wake wa dhati!