2013-12-01 13:32:35

Kongamano la kimataifa kwa ajili ya maendeleo dumifu na mshikamano Afrika


Mshikamano wa uchumi na maendeleo endelevu ni njia pekee ya kusonga mbele kwa Afrika; ni msisitizo uliotolewa Ijumaa, Novemba 29, wakati wa kazi za Kongamano la Kimataifa, linalo fadhiliwa na Taasisi ya Kipapa kwa ajili ya elimu ya Sayansi , kwa kushirikiana Taasisi ya “Sorella Nature”, Kongamano lililo fanyika katika jengo la Casina Pio IV ndani ya Vatican.

Kardinali Laurenti Monswengo Pasinya, Askofu Mkuu wa Kinshasa, akitoa mchango wake,katika Kongamano hili , kama kichocheo kwa ajili ya mustakabali wa Afrika,alisema, ni umuhimu sana, Afrika kuwa na mshikamano endelevu wa kudumu, katika mwanga wa hali halisi zinazo tajwa kwenye mafundisho ya kijamii ya Kanisa.
Kardinali alishutumu, kukosekana kwa nguvu ya usawa na usawa , ambavyo vimesababisha uwepo wa ustawi wa jamii bila ya mshikamano na umoja kijamii, kunako kuzwa na ukosefu wa ajira, kasa kwa lika la vijana. Na hili pia kuna dhoofisha mifumo ya demokrasia ambayo kwa sasa inapanuka lakini bila kuwa na sauti ya nguvu katika utoaji wa maamuzi, na hivyo kupoteza utambulisho wa utamaduni na misingi ya demokrasia, mbele ya unyonyaji wa nguvu wa rasilimali za madini, zinahitajika pia katika ustawi wa kijamii kwa vizazi vijavyo.
Kardinali Monsengwo, alitaja mahitaji muhimu kama lishe, elimu , afya, makazi na uhuru : kuwa masharti katika hali halisi Waafrika kupiga hatua za maendeleo, na isichukuliwe kama Waafrika ni wanufaikaji, lakini kama watendaji wa kuibadilisha Afrika.
Na Kardinali Giovanni Battista Re , kwa upande wake, aliufungua mkutano huo, kwa kusisitiza umuhimu wa kuwa na mawazo na utendaji kwa kwa ajili ya maendeleo endelevu.Na ili kuweza kupata matokeo halisi, Afrika inahitaji jitihada za kimataifa, uratibu na utaratibu wenye kuwashirikisha wanasiasa , asasi za kiraia, jamii ya kisayansi , mashirika ya kimataifa, viwanda na biashara . Kwa mujibu wa Kardinali Re, kwa wakati huu Afrika inaviishi vipindi vyote viwili kwa wakati mmoja, wakati wa ustawi na wakati mbaya zaidi.
Alibainisha ni nyakati bora, kwa kulinganisha kiwango cha hatua zilizopigwa katika kuboresha maisha, mafanikio na ustawi na kipindi cha nyuma, lakini pia wakati huu ni mbaya kwa njaa na utapiamlo unaosikika duniani na hasa Afrika , ikihamasishwa na kukosekana kwa usawa kati ya matajiri na maskini, na uhusiano kati ya mtu na viumbe , kwa sababu ya matumizi ya mabaya yanayo fanywa na nchi tajiri, na kama matokeo yake ni athari kwa mazingira, uwepo wa majanga ya asili kama vile mafuriko na ukame wa kukithiri.

Na Mmisionari Piero Gheddo , wa Taasisi ya Kipapa kwa ajili ya Shughuli za Kimisionari, alisema , maendeleo ya Afrika, yatafanikishwa na mambo mawili msingi Injili na Elimu.
Gheddo , alitoa mchango wake kwa uwazi zaidi, akirejea uchambuzi wa wamisionari toka nje ya Afrika wanaokaa barani Afrika, ambao wanataja sababu za Afrika kubaki nyuma kimaendeleo, kuwa ni pamoja na Madeni ya nje, ukosefu wa haki katika biashara ya kimataifa, mashirika ya kimataifa kufuja rasilimali za Afrika , kushamirishwa kwa biashara ya silaha kwa nchi na kati ya makundi mbalimbali ya kikabila, na kadhalika . Na wale wanao yajua kwa undani maisha ya kiafrika , wao wanataja Afrika inashindwa kupiga hatua za kasi katika maendeleo kutokana na sababu za kina za kihistoria, kiutamaduni na hata dini na elimu.
Kwa muhtasari, Wamisionari wanataja sababu kuu nne zinazo sababisha maendeleo duni barani Afrika: kwanza ni upagani , ambamo Waafrika wengi bado wamefungwa na ushirikina , kijicho , miiko, hofu ya ghasia , ibada katika roho wa vurugu na ukatili hata kwa binadamu. Pili ni suala la ujinga na ukosefu wa Shule . Watu wengi hawajui kusoma na kuandika kama zinazvyotaja takwimu za kijamii kwamba idadi hiyo ni kati ya asilimia zaidi ya 50. Licha ya uhaba wa shule hata zile zilizopo zinazingwa na Matatizo mengi , kama wingi wa wanafunzi kwa kila darasa, ukosefu wa vitabu , madaftari, zana elimu. Tatu ni matatizo ya ukabila na rushwa katika kila ngazi ya maisha ya umma, chini ya ngazi ya chini " na " kijeshi ni tabaka ya kwanza ya nguvu , kudhibiti siasa na uchumi. Na nne ni ukosefu wa historia na utamaduni thabiti wa mwafrika katika shughuli za maendeleo. Shughuli nyingi za maendeleo Afrika mara nyingi hupuuzwa au kuchukuliwa kama ni mambo ya wageni.
Wengine waliotoa mchangano wao katika Kongamano hili ni Askofu Mkuu Marcelo Sanchez Sorondo , Mkuu wa Taasisi ya Kipapa kwa ajili ya elimu ya Sayansi. Pia Waziri wa ushirikiano wa serikali ya Italia , Cecile Kyenge, aliyetunukiwa shahada ya heshima kutoka Chuo Kikuu cha Burkina Faso. Na Kardinali Óscar Andrés Rodríguez Maradiaga , Askofu mkuu wa Tegucigalpa.Pia Romano Prodi , mwakilishi wa Umoja wa Mataifa kwa Sahel, na Paolo Scaroni , Mkurugenzi Mtendaji wa Eni .








All the contents on this site are copyrighted ©.