Mkuu wa Jumuiya ya Taizè akutana na Papa Francisko
Brother Alois, Mkuu wa Jumuya ya Taize , Alhamis, alipokelewa Vatican na kukuana
na Papa Francisko akifuata nyayo za mtagulizi wake Brother Roger mwanzilishi wa Jumuiya
ya Taize, ambaye kila mwaka alifika Vatican kukutana na Papa.
Kwa mujibu wa
vyombo vya habari, ziara yake ya Brother Alyosius kwa Papa Francisko aliifanya katika
mazingira ya faragha, kama ilivyokuwa miaka ya nuuma alipokutana na Papa Benedikto
XV1. Brother Roger,wakati wake alikutana na Papa Yohane wa XXIII, Papa Paul VI na
Papa Yohane Paul II.
Alhamis iliyopita Brother Alosius katika maongezi yake
na Papa Francisko, alieleza jinsi wanavyowapokea vijana katika jumuiya ya Taize na
hija ya kiroho wanaoifanya kama hatua ya kuhamasisha vijana kiroho kutoka mabara yote.
Na Papa alizungumzia tukio hili la kiekumene la Taizé kwamba ubatizo, ni daraja linalo
waungnaisha wote na kuwapa nguvu za kutembea pamoja katika njia hii ya kiekumene.