Mkutano wa kimataifa dhidi ya adhabu ya kifo duniani
Jumuiya ya Mtakatifu Egidio yenye makao makuu yake mjini Roma, tangu mwaka 2002 imekuwa
ikiendesha kampeni dhidi ya adhabu ya kifo duniani inayoadhimishwa kila mwaka ifikapo
tarehe 30 Novemba. Hii ni tarehe ambayo Umoja wa Ulaya ulifuta adhabu ya kifo mjini
Toscana, kunako tarehe 30 Novemba 1786.
Tangu Mwaka 2002 Majiji na Miji ipatayo
80 inajiunga katika tukio hili linaloonesha umuhimu kwa Jumuiya ya Kimataifa kusimama
kidete kulinda na kutetea zawadi ya maisha. Mwaka huu, zaidi ya miji 1600 itashiriki
katika kampeni dhidi ya adhabu ya kifo na kati ya miji hii, kuna miji mikuu 70 kutoka
sehemu mbali mbali za dunia. Matukio mbali mbali yanatarajiwa kufanyika kwenye miji
hii kama sehemu ya maadhimisho ya kampeni dhidi ya adhabu ya kifo duniani.
Ijumaa
tarehe 29 Novemba 2013 kunafanyika mkutano wa kimataifa kuhusu kupinga adhabu ya kifo
unaohudhuria na wajumbe kutoka sehemu mbali mbali za dunia, lakini Bara la Afrika
kuna wawakilishi kutoka Tanzania, Msumbiji, Senegal, Burkina faso, Pwani ya Pembe,
Guinea Bissau, Guinea Conakry, Namibia, Niger, Togo, Ethiopia, Gabon, Rwanda na Morocco.
Hata
leo hii bado kuna nchi ambazo zinetekeleza adhabu ya kifo, ingawa kunako tarehe 20
Desemba 2012 Baraza kuu la Umoja wa Mataifa lilipisha kwa kura nyingi marathoni dhidi
ya adhabu ya kifo. Baadhi ya nchi hizi ni Gambia, Japn, India, Pakistan na Iraq na
China.