Imani si jambo binafsi, bali ni mwaliko kwa wote- Papa Francisko asema...
Imani si jambo binafsi, lakini ni mwaliko ulio wazi kwa watu wote, kumwabudu Mungu
mpaka mwisho wa maisha licha ya hatari ya kupambana na changamoto za maisha ya mateso
na kukatishwa tamaa na uovu.
Papa ameeleza na kuonya kwamba, kuna nguvu ya
kidunia, yenye kutaka kuifanya dini kuwa kama ni suala binafsi. Lakini Mungu, ambaye
ameshinda dunia , anaendelea kuipenda na kuutangaza uongofu wa kutembea katika njia
ya imani na Yesu Kristu katika ukamilifu na uaminifu wake,Papa alionya wakati wa Ibada
ya Misa, Alhamsi hii mapema asubuhi, katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta ndani ya
Vatican. Papa amesema Wakristo wanaoteswa leo hii , ni ishara ya mtihani, juu
ya ushindi wa Yesu dhidi ya shutuma na madhulumu aliyopambana nayo. Homilia ya
Papa ililenga katika mapambano ya mwisho, kati ya Mungu na maovu , kama masomo ya
liturujia katika kipindi cha kufunga mwaka yanavyo tahadharisha, kuwa macho na mitego
yote ya dhambi, ambayo Papa ameiita kuwa majaribu ya dunia. .
Majaribu ya kukabiliwa
na mvuto wa kumuasi Mungu kutoka kwa wale ambao wanaonekana kw amaovu wanayoyafanya
, kama vile wamemshinda Mungu, na kuonekana kuw ana maisha bora zaidi katika jamii,
wingi wa vitu na mali, zaidi ya wale wenye kumuamini Mungu. Lakini Papa anaeleza
kwa Muumini vitu na mali si kitu kwake, kwa kuwa havimpi tumaini la kudumu na ushindi
dhdi ya mauti, ushindi unaoelezwa katika rejea wazi ya ushindi na tumaini lililoletwa
na Yesu, aliye yashinda majaribu jangwani na kisha katika maisha yake ya umma,ambamo
alivumilia yote, matusi na Kashfa na kutoheshimiwa hadi kifo cha aibu msalabani.
Kifo kilichoonekana kama Mfalme wa Ulimwengu ameshindwa vita, lakini akadhihirisha
kuwa ni Mkuu wa amani kwa utukufu wa ufufuko wake, baada ya kulala kaburini kwa siku
tatu.
Papa Francisko amesema, hii inaonyesha hatua za maisha ya Kristu, katika
kufanikisha mageuzi duniani. Ni kuushupalia ukweli wa imani na kuvumilia yote katika
hali ngumu za manyanyaso na mateso. Papa alilenga moja kwa moja kwa katika somo la
Injili, ambamo Yesu, anatabiri kuharibiwa kwa mji wa Jerusalem na kunajisiwa kwa imani
. Papa Francis, amewatia moyo Wakristu kwamba, katika majaribu ya mateso na madhulumu
, hakuna sababu za kuwa na hofu au kuogopa kuuishi Ukristu kwa uaminifu, kw akuwa
kama ilivyokuwa wakati wa Yesu mateso namadholumu hayo yanamuimarisha muumini katikakutembea
karibu na Yesu kuielekea Jerusalem mpya ya milele. Yesu anawataka waamini wake kuwa
aminifu na kuvumilia, kama ilivyokuwa kwa Daniel , ambaye alikuwa mwaminifu kwa Mungu
wake na kuabudu Mungu mpaka mwisho kwa kuwa, aliyasadiki ahadi ya Mungu " hakuna unywele
wa kicha cha muumini utakao anguka bure"Hii ni ahadi ya Bwana, na tuombe neema na
majaliwa ya kusadiki hili, Papa Francisko ameomba.