Hakuna Ukristo wa kweli pasi ya kulifahamu Fumbo la Pasaka!
Tarehe 16 Novemba 2013 ni siku iliyoingia katika historia ya Jimbo Kuu la Dar es Salaam.
Katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Loyola, umati wa waamini wa Jimbo Kuu walikusanyika
katika kuadhimisha kilele cha Mwaka wa Imani.
Ibada ya kilele ilitanguliwa
na maandamano yaliyojaa shamrashamra ya waamini wengi wao wakiwa wameshika matawi
ya miti toka dekania zote saba za Jimbo. Maandamano haya ya kila dekania yaliingia
katika viwanja vya Loyola wakiwa wamebeba zana walizokabidhiwa kila dekania siku ya
kufungua Mwaka wa Imani. Zana hizi za kiimaani ni Msalaba wa Mwaka wa Imani, Bango
la Mwaka wa Imani na Bendera ya Mwaka wa Imani. Zana hili zilizungushwa katika kila
parokia, vigango, jumuiya na kila familia.
Ibada ya Misa ya kilele cha Mwaka
wa Imani iliongozwa na Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, akisaidiwa na maaskofu wasaidizi
Eusebius Nzigilwa na Titus Mdoe, pamoja na wakreli mia na siti na moja. Katika homilia
yake Mwadhama alisisitiza juu ya nafasi ya pekee ya Msalaba katika kuishi imani ya
kweli ya kikristo. “Bila Msalaba, hakuna imani ya kikristo” alisisitiza Mwadhama.
Katika Misa hii ya kilele watoto mia arobaini walibatizwa, wakiwakilisha watoto
elfu kumi waliobatizwa katika kipindi chote cha Mwaka wa imani. Mwisho wa ibada hii
Mwadhama alitoa baraka ya rehema kamili kwa waamini wote waliokuwa wamejiandaa kupokea
rehema kamili.
Katika adhimisho hili, kama ishara ya kuipokea kwa mikono miwili
Katekesimu ya Kanisa Katoliki katika maisha ya kila siku ya kichungaji ya Jimbo. Mwadhama
Polycarp Karidnali Pengo alizindua Katekesi ya Kanisa Katoliki iliyoandaliwa kwa kuwashirikisha
makatekista kwa ajili ya watoto walioko katika mafundisho ya Komunyo ya Kwanza.
Tukio
la pekee katika ibada hii, ni mvua kubwa iliyonyesha katikati ya ibada. Licha ya ukubwa
wa mvua na sehemu kadhaa za uwanja kujaa maji, waamini walibaki watulivu na kushiriki
kikamilifu ibada mpaka mwisho. Jambo hili lilimfariji kwa namna ya pekee Mwadhama
na kuwashukuru waamini wote ambao walionesha ukomavu wao, licha ya mvua hiyo.
Mwadhama
Pengo, aliwaasa waamini katika salamu zake, mwisho wa Misa hiyo kuwa kufunga Mwaka
wa Imani, si ndio mwisho wa imani, bali sasa kila mwamini anapaswa kuendelea kuishi
imani yake kwa namna bora zaidi, akiutazama Msalaba wa Kristo kama dira ya maisha
yake ya kila siku.