2013-11-28 11:20:13

Berlusconi avuliwa useneti


Bwana Silvio Berlusconi moja ya wanasiasa na wafanya biashara mashuhuri nchini Italia, Jumatano tarehe 27 Novemba 2013 Bunge limepiga kura ya kumvua madaraka ya Seneti, kumbe kuanzia sasa si Seneti tena wa Italia baada ya kupatikana na hatia ya kukwepa kulipa kodi halali kwa Serikali ya Italia.

Wananchi wengi wa Italia wameupokea uamuzi huu kwa hisia mchanganyiko wengine kwa kusema kwamba, haki imetendeka na kwamba hiki ni kielelezo cha utawala wa sheria ambayo kila mwananchi anapaswa kuifuata. Baadhi ya wananchi wanasema, Bwana Berlusconi anaonewa na majaji ambao wamekuwa wakimbambikia kesi kibao, pengine ni kati ya wanasiasa wachache wa Italia wenye kesi nyingi mahakamani!

Kwa upande wake, Berlusconi anasema, uamuzi wa Bunge la Italia kumvua madaraka ya Usenati ni maombolezo makubwa kwa kifo cha demokrasia ya Italia, maneno ambayo yamewachefua wanasiasa wengi nchini Italia kwa kusema kwamba, ni maneno ya mtu aliyekata tamaa katika maisha.







All the contents on this site are copyrighted ©.