2013-11-27 15:49:52

Papa akutana na watoto wenye makuzi hasi.


Jumatano hii, kabla ya kutoa Katekesi yake kwa mahujaji na wageni , Baba Mtakatifu Francisko, alikutana na watoto wenye maradhi mabaya ya ukuaji hasi, wakiwa na famiia zao , kundi la watu wapatao 170. Hii haikuwa mara ya kwanza kwa Papa kukutana na watoto wenye maradhi mabaya.

Inakumbukwa tarehe 4 Oktoba akiwa Asissi Italia, Papa alikutana na watoto walemavu na wagonjwa, kama ilivyokuwa imeandaliwa katika Taasisi ya Serafico ambayo kila mwaka tangu 1871, kwa msaada wa vijana wa kujitolea huwapokea watoto walemavu kutoka sehemu zote za Italia. Na tarehe 31 Mei Papa alikipokea kikundi cha watoto 22 wagonjwa mahututi kama ilivyoandaliwa na Kitengo cha tiba kwa watoto cha Hospitali ya Policlinico Gemelli Roma.
Kwa tukio la Jumatano hii , Papa Francisko aliongoza sala ya Maria , akiwa pamoja na wazazi na jamaa za watoto hao, na baadaye aliwapa baraka zake na kuwakumbatia kwa upendo akisema, huu ni wakati wa kusema Yesu njoo kati yetu, tukukumbatie. Na aliwaomba watoto hao wasimsahau Papa katika sala zao.
Wawakilishi wa viwanda -Argetina Na mapema siku ya Jumanne , Papa Francisko , akiwa katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta, alikutana na kundi la makatibu wawakilishi wa wafanyakazi viwandani ktutoka Argentina. Katika salamu zake , Papa alitoa kwao mwaliko wa kujibidisha kushiriki katika juhudi zinazolenga kukuza maadili ya kitamaduni na amani. alieleza hili akirejea kumbukumbu mti wa mzeituni uliopandwa na Kardinali na Askofu Mkuu wa Buenos Aires mwaka 2000 katika uwanja wa Plaza de Mayo, kama ishara ya amani.
Papa amesema, ishara hiyo ya mzeituni, ni uvuvio wa dhamira safi hasa mashuleni, na mtandao wote wa shule duniani kote, na juhudi za mipango ya kukuza kazi za kitume zilizoanzishwa na yeye Papa wakati ule akiwa Askofu Mkuu Jorge Mario Bergoglio, Askofu Mkuu wa Buenos Aires, mji mkuu wa Argentina.








All the contents on this site are copyrighted ©.