Maisha ni maandalizi ya uzima wa milele! Papa Francisko asema..
Jumatano hii , Baba Mtakatifu akitoa mafundisho yake kwa mahujaji na wageni waliokusanyika
katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, wapatao 50,000, kwanza aliwashukuru
na kuwapongeza kwa moyo wao wa kupenda kusikiliza mafundisho ya Papa licha ya hali
ya baridi iliyokuwepo uwanjani hapo.
Katika hotuba yake, Papa alieleza kwamba
leo anakamilisha katekesi zake juu ya sala ya imani, sala ya Nasadiki, ambayo amekuwa
akiizungumzia katika kipindi cha maadhimisho ya mwaka wa imani, ulio kamilika Jumapili
iliyopita.. Leo Papa ametafakari juu ya Ufufuko wa Mwili, kama iiivyo katika mafundisho
ya Kateksimo ya Kanisa Katoliki.......
Alianza kusema, ndugu zangu wapendwa,
napenda kuikamilisha katekesi hii ya Imani kwa kutafakari juu ya ufufuo wa mwili.
Imani ya Kikristo hutumulikia katika fumbo la kifo na matumaini katika ufufuko. Kifo
ni changamoto kwetu sote. Mbali na imani kwa Mungu, na muono wa maisha kama ni hali
katika uwepo wa dunia , kifo kinaonekana kuwa ni janga la kutisha , na kutufanya tupoteza
maana yake, kikileta hofu kali ya kutaka kujiweka mbali nacho. Lakini kumbe binadamu
aliumbwa na jambo moja kuu, ambalo humpatia hamu ya kuwa katika uwepo usio na mipaka,
umilele.
Papa aliendelea kufundisha kwamba, Ufufuko wa Kristo si tu hutuonyesha
uwepo wa maisha zaidi baada ya kifo, lakini pia hutuonyesha maana ya kweli ya kifo,
kwamba, tunakufa kwa ajili ya kuishi upya: iwapo maisha yetu haya ya nyama na damu
yatakuwa katika muungano na upendo na Mungu. Katika kuishi na Mungu, tunapata uwezo
wa kuachana na maisha haya katika hali ya utulivu na ujasiri wa kujiweka katika mikono
ya Mungu wakati wa kifo chetu.
Papa alikumbusha , Bwana wetu mara nyingi anatuambia
kuwa waangalifu namanabii wa uongo, akijua kwamba , maisha yetu katika dunia hii ,
ni kwa ajili ya maandalizi ya maisha yajayo. Kama tunabaki karibu naye, hasa kwa
njia ya kuwapenda maskini na kuwa na mshikamano na wahitaji, hakuna haja ya kukiogopa
kifo, bali ni kukipokea kifo kwa furaha wakati mlango wa mbinguni upofunguliwa kwa
ajili ya kuingia katika furaha ya uzima wa milele.