Papa Francisko atoa "Encyclical" yake ya kwanza: “Evangelii Gaudium”
Askofu Mkuu Claudio Celli , Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Mawasiliano Jamii,
Jumanne 26 Novemba 2013, amewasilisha kwa wanahabari, waraka wa kitume wa kwanza wa
Papa Francisko juu ya utangazaji wa Injili katika Dunia ya leo. Askofu Mkuu Celli,
akiuzungumzia waraka huu, alitaja mambo mawili kwanza mtindo na lugha iliyotumika
akisema kwamba, mna tabia ya kina yenye kutoa msukumo wa kichungaji. Kama Papa Francisko
yeye mwenyewe anavyosema, kwamba, anatamani kuufikisha ujumbe huu kwa Wakristu wote,
kuwakaribisha katika hatua mpya ya uinjilishaji. Askofu Mkuu Celli anasema ,
hivyo katika kuusoma waraka huu, mnatoa changamoto kwa wachungaji, kufanya mazungmzano
na tafakari na Walei. Papa amehimiza utumiaji wa lugha nyepesi na unyenyekevu kama
inavyojionyesha katika hotuba na homilia zake katika kipindi hiki cha miezi michache
ya utawala wake. Askofu Mkuu Claudio ametaja kipengere kingine kilicho sisitizwa
na Papa katika waraka huu kuwa ni jukumu la mawasiliano katika hatua hii mpya ya uinjilishaji.
Papa anataka kuonyesha, njia ambamo Kanisa linatakiwa kutembea katika miaka ijayo.
Askofu Mkuu Celli anasema, ni dhahiri , zaidi ya yote, Papa Francisko anafahamu
kile kinachoendelea katika ulimwengu wa leo , hasa katika uwanja wa afya, elimu na
mawasiliano. Kwa ufahamu na utambuzi alionao katika maendeleo na mafanikio ya mtu
kwa wakati huu, hasa katika mambo yanayohusiana na ubunifu dhahiri teknolojia , anasema,
tuko katika enzi ya ubunufu, maarifa na mawasiliano, chanzo cha aina mpya ya nguvu.
Katika mtazamo huo, Papa ametahadharisha hasa katika utoaji wa homilia akisema,
inafaa kujua tatizo, si tu kujua nini cha kusema lakini hasa kwa namna gani kutakuwa
na mwendelezo wake. Kwa ajili hii Papa Francisko, anasisitiza mahubiri mepesi yanayoweza
kutoa picha nzuri kwa wanaosikiliza. Mahubiri mazuri nyeye kutoa wazo , hisia, picha.
Pia Papa anakumbusha daima suala la lugha , akikumbusha umuhimu wa unyenyekevu
katika lugha inayotumika. Ni lazima kuwa na lugha nyepesi ya kueleweka na si kuzunguka
zunguka. Askofu Mkuuu Claudio Celli, amekamilisha pamoja na maelezo mengine alikamilisha
hotuba yake kwa kutoa mtazamo zaidi wa Papa Francisko , katika mawasiliano kwenye
shughuli za Kanisa , akisema ni lazima, mawasiliano yaonyesha maana ya shughuli za
Kanisa. Na hivyo wahusika wanapaswa kuwa na ujasiri wa kupata ishara mpya , alama
mpya, nyama mpya kwa ajili ya maambukizi ya neno, aina mbalimbali za uzuri kuwa wazi
wenyewe katika nyanja mbalimbali za kitamaduni. Na hii ni changamoto, inayotolewa
na Papa Francisko, kwa kila muumini wa kanisa. .