Mkutano wa Syria kimataifa sasa kufanyika tarehe 22 Januari 2014
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Ban Ki-Moon ametangaza kwamba, mkutano wa kimataifa
unaotarajiwa kuzungumzia kuhusu hali ya amani na usalama nchini Syria, utafanyika
tarehe 22 Januari 2014 mjini Geneva. Mkutano huu ni daraja la kipindi cha mpito nchini
Syria ili kujenga na kuimarisha uhuru na utu wa wananchi wa Syria ambao kwa miezi
ya hivi karibuni wameendelea kukumbana na majanga ya maisha.
Ulinzi na usalama
ni kati ya vipaumbele vinavyotolewa na Umoja wa Mataifa kwa wakati huu. Wadau wakuu
katika mkutano wa Geneva ambao ulikuwa unatarajiwa kufanyika mwishoni mwa Mwezi Novemba,
2013 walikuwa ni Marekani na Russia, umefutwa baada ya pande zinazohusika kushindwa
kuafikiana katika masuala nyeti! Iran na Saud Arabia zinatarajiwa kushiriki katika
mkutano huu kadiri ya taarifa za kidiplomasia.