Wakristu wanao teseka leo hii, ni ushuhuda wa kuigwa na wote katika kufanya uchaguzi
thabiti.
Jengeni matumaini kwa Bwana, hata katika hali ngumu, Papa amehimiza wakati wa Ibada
ya Misa ya asubuhi Jumatatu hii katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta mjini Vatican.
Papa alisisitiza kwamba Wakristo wameitwa kufanya maamuzi thabiti , kama yanavyo fundisha
maisha ya mashahidi wa dini wa kila wakati. Hata leo, alibainisha, kuna wake kwa waume
wanao teseka kwa sababu ya imani yao kwa Kristu. Na hivyo wao ni mfano kwetu wa kuiga,
kwa ajili ya kupata nguvu za kujikabidhi kwa Bwana bila kujibakiza. Papa aliendelea
kufundisha kwamba, kumchagua Kristu, hakuna ukomo. Alieleza hilo akingalisha katika
somo la Kitabu cha Nabii Daniel, na Injili : ambamo vijana Wayahudi watumwa katika
mahakama ya Nebukadreza na mjane aliyekwenda katika hekalu kumwabudu Bwana. Katika
kesi zote, Papa anaona, hapakuwa na ukomo wa hali. Mjane katika hali ya umaskini na
vijana katika hali ya utumwa, wote walijikabidhi kwa Bwana . Mjane aliweka vyote alivyokuwa
navyo katika hazina ya Hekalu, ambapo kwa vijana walibaki aminifu kwa Bwana, hata
katika hatari ya maisha. Papa aliendelea kusema, katika hali za wote, mjane na
vijana – hawakujali hatari za maisha zilizokuwa mbele yao. Walimchagua Bwana kwa
moyo moja, bila wasiwasi na bila upungufu. Kwao Bwana alikuwa ni juu ya yote juu.
Walitambua Bwana wao ni Mungu na kwake walijikabidhi wenyewe. Na hii hawakufanya kwa
sababu za kujitafutia sifa bandia , lakini walifanya hivyo kwa kutambua kwamba, Bwana
ndiye mkuu wa yote. Walijua kwamba Bwana ni mwaminifu. Na ndivyo tunavyotakiwa nasi
pia kufanya. Ni kumtegemea Bwana kwa uaminifu na imani kwamba daima yupo, kwa
sababu Bwana hawezi kubadilika kubadilika na kujikana mwenyewe. Imani hii katika Bwana
Papa Francisko aliongeza, huongoza katika maamuzi thabiti ya kumchagua Yeye kuwa ndiye
Bwana wa Yote, Yeye ni mwaminifu, katika katika mambo yote madogo , makubwa na hata
magumu.
Papa alieleza na kuitazama historia ya kanisa kwamba, historia yake
inaonyesha wanaume, wanawake, wazee, vijana, waliofanya uchaguzi huu, kama tunavyo
sikia katika vyombo vya mawasiliano au kusoma katika magazeti juu ya maisha ya mateso
yanayokabili hata leo hii, Wakristo katika maeneo mbalimbali duniani.
Wakristu
hao wanaoishi nasi katika wakati huu, ni mfano hai kwetu, wenye kutuhimiza pia sisi,
kuiweka hazina yetu ndani ya kanisa, ili kwamba, ambamo Bwana yumo ndani mwake.
Ushuhuda wa Wakristu hawa wateswa, unashuhudia neema ya ujasiri wa kusonga mbele katika
maisha ya Kikristo , katika hali ya kawaida , maisha magumu na hata katika mazingira
hatarishi . Ni kuwa na Maamuzi thabiti kwa Bwana.