2013-11-25 10:47:11

MDM yakitoa jasho chama cha Frelimo nchini Msumbiji!


Tangu baada ya Msumbiji kujinyakulia uhuru wake kutoka kwa Mreno, Chama cha Frelimo kimekuwa kikishinda kwa kishindo, lakini uchaguzi wa serikali za mitaa uliohitimishwa hivi karibuni nchini humo unaonesha kwamba, kuna mabadiliko makubwa miongoni mwa wapiga kura kwa watu kuonesha upendeleo kwa Chama cha Mageuzi Msumbiji, MDM.

Hiki ni chama ambacho ni cha tatu kwa ukubwa baada ya Renamo ambacho kilisusia uchaguzi huo na kutishia kurudi tena msituni kuendesha mapambano ya silaha. Wachunguzi wa masuala ya kisiasa nchini Msumbiji wanasema kwamba, Frelimo itashinda kwa asilimia kubwa, lakini kwa sasa inaanza kupata wapinzani wanaoendelea kujiimarisha katika uwanja wa demokrasia hasa katika miji mikubwa nchini Msumbiji.







All the contents on this site are copyrighted ©.