2013-11-21 12:03:21

Askofu Thomas Msusa ateuliwa kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Blantyre, Malawi


Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Askofu Thomas Msusa kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Blantyre, Malawi. Kabla ya uteuzi huu, Askofu Msusa alikuwa ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Zomba.

Askofu mkuu mteule alizaliwa kunako tarehe 2 Februari 1962 Wilyani Mangochi. Baada ya masomo na mjiundo yake ya Kipadre, akapewa daraja takatifu la Upadre hapo tarehe 3 Agosti 1996. Tarehe 16 Januari 2004 akateuliwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Zomba na kuwekwa wakfu kuwa Askofu hapo tarehe 17 Aprili 2004.







All the contents on this site are copyrighted ©.