2013-11-18 09:21:15

Zuieni ajali barabarani kwa kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani!


Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana, Jumapili iliyopita, tarehe 17 Novemba 2013, aliwasalimia waamini na mahujaji kutoka ndani na nje ya Italia. Amewakumbuka Wakristo kutoka Eritrea waliokuwa wanaadhimisha kumbu kumbu ya Mtakatifu Mikaeli.

Jumapili iliyopita, nchini Italia wameadhimisha Siku ya Usalama Barabarani kwa kuwakumbuka na kuwaombea watu waliopatwa na ajali barabarani. Baba Mtakatifu amewahakikishia uwepo wake wa karibu kwa njia ya sala. Anaendelea kuhimiza umuhimu wa kuzuia ajali kwa kuwa makini, wanyofu pamoja na kuheshimu sheria na kanuni za Usalama Barabarani, ili kulinda maisha ya mtu binafsi pamoja na yale ya watumiaji wengine wa barabara.

Mwishoni, kama sehemu ya mwendelezo wa Maadhimisho ya Mwaka wa Imani, Baba Mtakatifu amewapatia waamini dawa maalum ya maisha ya kiroho, ambayo waamini na mahujaji waliokuwepo kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro wamegawiwa.







All the contents on this site are copyrighted ©.