2013-11-18 14:35:23

Waziri mkuu wa Bahamas akutana na Papa Francisko mjini Vatican


Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu tarehe 18 Novemba 2013 amekutana na kuzungumza na Waziri mkuu wa Bahamas Perry Gladstone Christie na ujumbe wake ambao pia umekutana na viongozi waandamizi kutoka Vatican chini ya Askofu mkuu Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican.

Viongozi hawa wawili wamejadili pamoja na mambo mengine kuhusu uhamiaji na mchango wa Kanisa katika maendeleo ya wananchi wa Bahamas, hususan katika sekta ya elimu na kwamba, wameonesha utashi wa kutaka kuimarisha ushirikiano wao katika medani mbali mbali za maisha.







All the contents on this site are copyrighted ©.