Italy na Vatican watoa angalisho kwa wimbi la wahamiaji Italia
Alhamis wakati wa ziara ya Papa kutembelea Ikulu ya IItalia "Quirinale" alikuwepo
pia Waziri Mkuu wa Italia Enrico letta, akiongozana na Katibu Mkuu wake Phillip
Patroni Griff,ambao, baadaye waliutumia muda wao, kukutana na Kaimu Katibu Mkuu wa
Vatican Askofu Mkuu Angelo Becciu, na Askofu Mkuu Domenico Mamberti , Katibu wa
Vatican katika Mahusiano na Nchi zingine, akiwepo pia Rais wa Baraza la Maaskofu la
Italia, Kardinali Angelo Bagnasco. Mazungumzo ya viongozi hao , yalilenga zaidi
suala la uhamiaji, hasa katika mwanga wa majanga ya hivi karibuni, na hali ngumu ya
maisha ya wahamiaji na wakimbizi katika kituo cha wakimbizi cha Lampedusa. Waziri
Mkuu wa Italia, alifanya rejea katika kile alichokishudia wakati wa ziara yake huko
Lampedusa, ambako Papa Francisko pia alifanya ziara ya kujionea mwenyewe kinachoendelea.
Waziri Mkuu wa Italia , Mheshimiwa Letta katika maelezo yake , aliitumia nafasi
hiyo, kutoa taarifa mpya ya kile kinachoendelea katika kituo hicho cha wakimbizi na
wahamaiji cha Lampedusa akisema kwamba, serikali yake imechukua hatua mpya za utendaji
katika mwambao wa bahari ya Menditterania kwa ajili ya kuzuia maisha ya watu kutumbukia
baharini kama ilivyotokea hivi karibuni. Kati ya hatua zilzo imarishwa ni kuwatia
mbaroni wote wanao bainika kufanya biashara haramu ya kusafirisha watu kwa vyombo
dhaifu baharini, kinyume cha sheria . Serikali ya Italia na Vatican , kwa pamoja
pia katika mazungumzo hayo ya Alhamis, walionyesha kujali kinachoendela Syria na Libya,
wakiona kwamba, maafa yanayotokea katika bahari ya Meditterania ni matokeo ya hali
za wasiwasi na vurugu za kivita vinavyo shamiri katika mataifa hayo , na hivyo watukuingiwa
na wasiwasi wa usalama wa maisha na hivyo kuamua kuondoka bila ya kujali yatakayo
kumbana nayo huko wanako elekea. Na hivyo kukuza wimbi wa uhamiaji. Na hivyo, kwa
ajili hiyo, Italia na Jimbo Takatifu, wanalitazama tatizo hilo kwa utendaji makini
na wa nguvu.