Wakuu wa Jumuiya ya Madola wanakutana nchini Sri Lanka
Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania ameondoka jioni ya leo tarehe 13 Novemba,2013
kuelekea Colombo , Sri-Lanka kuhudhuria kikao cha siku tatu (3) cha Wakuu wa Nchi
za Jumuiya ya Madola (Commonwealth Heads of Government Meeting – CHOGM) kinachotarajiwa
kuanza tarehe 15-17 November,2013. Sri-Lanka inachukua uenyekiti wa Jumuiya ya Madola
kwa kipindi cha miaka miwili ijayo kutoka Australia.
Pamoja na Kikao cha CHOGM
Rais Kikwete anatarajia kuhudhuria kikao cha viongozi na baadhi ya wafanyabiashara
. Kwa mara ya kwanza Malkia wa Uingereza hatahudhuria Kikao cha Sri-Lanka na badala
yake atawakilishwa na mwanae Prince Charles.
CHOGM ni Kikao kinachofanyika
kila baada ya miaka miwili ambacho ujumbe wa mwakani “Growth with Equity: Inclusive
Development” ujumbe ambao unasisitiza Ukuaji na Maendeleo yatakayokuwa na faida
na usawa kwa jamii nzima kwa lengo la kupunguza pengo lililopo kati ya maskini na
matajiri katika jamii. Pamoja na agenda hiyo, viongozi hao watapata nafasi ya kuzungumzia
hali ya kisiasa na kiuchumi katika nchi za Jumuiya ya Ulaya, mabadiliko ya hali ya
hewa na biashara baina ya mataifa. Kikao cha viongozi kitafanyika baada ya kufanyika
kwa baadhi ya vikao vya makundi mbalimbali katika Jumiya ikiwemo Vijana, Wafanya biashara,
makundi maalum na cha Mawaziri.
Kifo cha Dkt. Mvungi chamshtusha
RaisKikwete
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya
Mrisho Kikwete ameshtushwa na kufadhaishwa na taarifa za kifo cha Mjumbe waTume ya
Mabadiliko ya Katiba, Dkt. Sengondo Mvungi kilichotokea Jumanne, Novemba 12, 2013
kwenye Hospitali ya Milpark, Johannesburg, Afrika Kusini.
Katika salamu za
rambirambi ambazo amemtumia Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Joseph SindeWarioba, Rais
Kikwete amesema kuwa amepokea kwa mshtuko mkubwa na fadhaha taarifa za kifo cha Dkt.
Mvungi. “Kwa hakika ni taarifa iliyonisumbua na kunipa huzuni nyingi.” Rais Kikwete
amesema kuwa hakuna shaka kuwa katika maisha yake Dkt. Mvungi ametoa mchango mkubwa
katika maendeleo ya Tanzania kwa namna mbalimbali na kuwa kifo kimemfika wakati Taifa
la Tanzania lilikuwa bado linahitaji busara, hekima na mchango wake katika mchakato
mzima wa kusaka Katiba mpya.
“Kuanzia alipokuwa mwandishi wa habari katika
Magazeti ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya Uhuru na Mzalendo, hadi uhadhiri wake katika
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, hadi uwakili katika Kampuni ya South Law Chambers, hadi
uongozi wake katika Chama cha NCCR-Mageuzi, hadi uamuzi wake wa kugombea Urais wa
Tanzania mwaka 2005 na sasa akiwa Mjumbe wa Tume ya Katiba, Dkt. Mvungi ametoa mchango
wake mkubwa sana katika maendeleo ya nchi yetu. Na hili hatutalisahau,” amesemaRaisKikwete.
“Kwa
masikitiko makubwa, nakutumia wewe Jaji Joseph Warioba, Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko
ya Katiba salamu za rambirambi za dhati ya moyo wangu nikiombeleza kifo cha Dkt. Mvungi.
Nakupa pole nyingi wewe Mwenyekiti, wajumbe wa Tume na wafanyakazi wote wa Tume kwa
kuondokewa na mwenzenu. Naungana nanyi kuombleza msibahuo mkubwa.”
“Aidha,
kupitia kwako, natuma pole nyingi kwa wana-familia, ndugu, marafiki nan majirani wa
Dkt. Mvungi kwa kuondokewa na mhimili,msimamizi wafamilia na ndugu. Wajulishe kuwa
niko nao katika msiba huu mkubwa.Wajulishe kuwa msiba wao ni msiba wangu pia. Muhimu
waelewe kuwa binafsi naelewa machungu yao katika kipindi hiki kigumu na namwomba Mwenyezi
Mungu awape subira waweze kuvuka kipindi hiki kigumu kwa sababu yote ni mapenzi yake.”
Amemalizia
Rais Kikwete: “Napenda kuungana nao katika kumwomba MwenyeziMungu, Mwingi wa Rehema,
aiweke mahali pema roho ya Marehemu Dkt. Sengondo Mvungi. Amina.”