Rais Giorgio Napolitano ampokea Papa katika jengo la Ikulu ya Italia.
Rais Giorgio Napolitano,Alhamis hii 14 Novemba 2013, majira ya saa nne alimpokea
Papa Francisko, aliyemtembea akiwa katika makazi ya Ikulu ya Italia inayojulikana
kwa jina la Quirinale, yaliyoko katikati ya jiji la Roma.
Rais Napolitano
katika hotuba yake ya mapokezi, hakuficha furaha yake ya kutembelewa na Papa akisema
anaona kama ni upendeleo fulani, na pia ugeni wake ni ushuhuda wa mwendelezo wa historia
ya muda mrefu katika mahusiano mazuri kati ya Rais wa Italia na Mkuu wa Kanisa Katoliki
la Ulimwengu, yaani Papa .
Na kwamba uwepo wa uwakilishi muhimu wa viongozi
wa Jamhuri ya Italia na taasisi zingine za serikali na mashirika ya kijamii, ulimwengu
wa utamaduni na dunia Katoliki , ni ishara wazi kwamba, inawezekana pia kuwa na mshikamano
wa karibu zaidi katika utendaji kwa ajili ya kusaidia watu maskini na wanaoteseka
kwa saba bu mbalimbali hasa majanga asilia, na mabavu mengine yaliyo nje ya uwezo
wao.
Rais Napolitano alitoa shukurani zake kwa Papa Francisko akisema, watu
wote - waumini na wasio waumini, wanaguswa na hotuba za Papa ambazo anazitoa kwa maneno
mepesi lakini yenye nguvu. Na wengi wameweza kupata mwamko wa kuona ukosefu au udhaifu
katika ushupavu, wa kupambana na changamoto za dunia, ambazo viongozi wengi,wanapenda
kujiweka mbali nazo na kuona kama si jukumu hilo, hasa kutokana na mashaka na wasiwasi
wa hali nchi zao kwa baadaye, iwe kisiasa au kitamaduni na hata kiimani.
Lakini
kwa hotuba zake Papa Francisko na watangulizi wake, pamoja na kusoma upya yaliyomo
katika waraka wa Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican, wameweza kuangaziwa upya na roho
wa Injili kwamba uwajibikaji wa kanisa katika masuala ya Kijamii ni kutetea tunu
msingi za ubinadamu kwa watu wote.
Na hivyo, watu wengi sasa wanaona fukuto
la matarajio mpya, katika mazungumzano na watu mbalimbali , hasa zaidi na wapinzani,
kwamba , ni muhimu kuwa na mahusiano ya karibu na kufanyakazi pamoja kwa ajili ya
udumishaji yaliyo mema kwa watu wote, kama ambavyo,Papa Francisko, amekuwa ukisistiza
katika hotuba zake, kwamba ni lazima kujitahidi kujenga ushirikiano wa karibu ,
kwa ajili ya kupambana na changamoto za kipekee za kisasa, na hasa katika ujenzi wa
mustakabali, kupitia uhamasishaji wa dhamiri na nishati na zaidi ya yote maadili....
Na kwamba Papa Francisko,amekuwa ni mfano mzuri wa kuigwa na viongozi katika utimizaji
wa ahadi wanazo toa.