2013-11-14 15:56:34

Papa atembelea Ikulu ya Italia - "Quirinale"


Baba Mtakatifu Francisko Alhamis hii 14.11.2014 majira ya saa nne, kwa mara ya kwanza tangu kuwa Papa mwezi March mwaka huu, alifanya ziara rasmi, kumtembelea Rais wa Italia, Mheshimiwa Giorgio Napolitano, aliyekuwa akimsubiri katika jengo la Ikulu la Qiurinale. Papa amefanya ziara hii Ikulu kama kulipa fadhila kwa Rais Giorgio ambaye alimtembelea Papa June 8, mwaka huu. Papa Francisko ametembelea makazi haya ya Rais wa Italia, ya Quirinale, ambayo awali yalikuwa ni makazi ya Papa kwa karne nyingi hadi 1870.

Baada ya ukimya wa miaka mingi, ziara za Papa kutembelea Quirinale, zilianzishwa mwaka1939 na Papa Pius X11 alipomtembea Mfalme wa Italy Emmanuel 11 aliyekuwa akiishi katika jengo hilo. Na Mapapa waliofuatia wakaiga pia utamaduni huu wa kutembelea Ikulu wa Italia kama ishara ya mahusiano mazuri.

Hotuba ya Papa Francisko kwa Rais Napolitano , imegusa matatizo ya kijamii na kiuchumi yanayotendea vibaya taifa la Italia, kama vile ukosefu wa ajira, na hivyo ametoa wito kwa taasisi za serikali, kutenda kwa ufanisi zaidi kwa ajili ya kusaidia familia. Na kwamba yeye mwenyewe anapenda kufanya safari za kugonga katika kila mlango wa kila nyumba, kwa nia ya kufikisha maneno ya uponyaji wa injili.

Papa Francisko ameitaja ziara yake hii katika makazi ya Rais wa Italia, kuwa ni ushuhuda wazi unaothibitisha uwepo wa mahusiano mazuri kati ya Nchi ya Italy na Nchi ya Jimbo la Takatifu , huku akikumbuka ziara ya mtangulizi wake, Mstaafu Bendikto XV1, katika Ikulu hiyo ya Quirinale YA mwaka 2008.

Papa Francis alisema, katika majukumu yao tofauti, Kanisa na serikali, lakini bado wanayo mengi ya kushirikishana kwa ajili ya ufanikishaji maisha bora katika hali za kawaida za kijamii, na hasa masuala yanayoleta uchungu zaidi katika maisha kama vile mgogoro wa kiuchumi, na ukosefu wa ajira na matokeo yake mabaya. Na hivyo akahimiza kila mmoja kurudufu jitihada ili kupunguza Madhara ya haya.

Na kwamba, ni wajibu mkubwa wa Kanisa, Papa aliendelea, kushuhudia wema na huruma ya Mungu na kuhimiza watu kutoa jibu la ukarimu wenye mshikamano kwa wahitaji . Kwa njia hii , inawezekana kujenga jamii iliyo na haki zaidi na ubindamu zaidi na katika kukuza maendeleo endelevu na afya.

Alieleza kwa kuikumbuka ziara za kichungaji kwa visiwa vya Lampedusa na Sardinia na mji wa Assisi , ambako alishuhudia mwenyewe hali na mateso na mahangaiko ya watu wanaotafuta ahueni katika maisha . Pia hakusahau kutaja kitengo cha familia ambacho nacho kwa wakati huu kinakabiliwa na changamoto kali.

Kwa ajili ya familia, Papa ametoa wito kwa kila mtu , kusaidia kitengo cha familia , ili kiweze kupendwa, kuthaminiwa na kulindwa" hivyo kuweza kutimiza kazi yake muhimu katika jamii.


Na alimalizia kwa kuonyesha tumaini lake kwamba, Italia itaweza kurejesha moyo wake katika kazi za ubunifu na maelewano, ili kwamba kila wakazi wote wa Italia,waweze kufurahia ustawi wenye kuheshima utu na haki kwa kila mtu. .









All the contents on this site are copyrighted ©.