Onesheni mshikamano wa upendo kwa wananchi wa Ufilippini kwa kuchangia kwa hali na
mali!
Baraza la Maaskofu Katoliki Italia limeupokea wito na mwaliko wa Baba Mtakatifu Francisko
anayewataka waamini na watu wote wenye mapenzi mema kujiunga katika mapambano yanayopania
kuokoa maisha ya wananchi wa Ufilippini waliokumbwa na majanga hivi karibuni kama
njia ya kuonesha mshikamano wa upendo kwa hali na mali.
Baraza la Maaskofu
Katoliki Italia linatangaza kwamba, tarehe Mosi, Desemba 2013 itakuwa ni siku maalum
ya mshikamano na ananchi wa Ufilippini. Waamini na watu wenye mapenzi mema wanaalikwa
kuchangia kwa hali na mali katika jitihada za kuokoa maisha ya watu wengi wanaohitaji
msaada wa dharura kwa sasa. Hadi sasa Shirika la MIsaada la Kanisa Katoliki Italia
limekwishachangia jumla ya Euro 1000, 000 kusaidia wananchi wa Ufilippini.