2013-11-14 11:12:38

Maafa nchini Somalia!


Zaidi ya watu 300 wanasadikiwa kufariki dunia nchini Somalia mwishoni mwa juma kutokana na mvua kubwa iliyonyeesha katika mkoa wa Puntland, Kaskazini Mashariki wa Somalia, lakini jambo la kusikitisha ni kuona kwamba, vyombo vingi vya habari haviguswa na maafa haya kana kwamba, hakuna kitu chochote kilichotokea.

Baadhi ya watu wanasema, hii ni kutokana na mazoea, vifo vya watu nchini Somalia linaonekana kuwa ni jambo la kawaida, lakini haipaswi kuwa hivi! Maisha ya mtu ni zawadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Taarifa zinaonesha kwamba, kuna idadi kubwa ya watu ambao hawajulikani waliko na inahofiwa kwamba, pengine wamekufa maji. Mafuriko haya yamesababisha maafa makubwa ambayo pengine yamemezwa na habari za kusikitisha za tufani iliyopiga nchini Ufilippini.







All the contents on this site are copyrighted ©.