Papa Francisko mara baada ya Mafundisho yake ya Jumatano , akiwa katika uwanja wa
kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, alirudia kuiomba dunia, kutoa kwa ukarimu wote, msaada
kwa watu walio sasa katika mahangaiko makubwa kutoka na maafa yaliyo nje ya uwezo
wao, hasa huko Ufilipino. Na pia aliionyesha kuguswa na janga la wanafunzi waliofariki
huko Dameski kwa basi lao kulipuliwa na bomu wakati wakirejea toka shule na kusababisha
maisha ya wanafunzi kadhaa na dreva wao kufariki na wengine wengi kujeruhiwa karibuni
huko Dameski. Kwa majonzi makubwa, Papa alikemea utendaji huo akisema kamwe na
isitokee tena. Papa amemwomba Mwenyezi Mungu ayaepusha majanga haya yenye kuangamiza
roho za binadamu, alizoziumba yeye mwenyewe.