2013-11-12 08:06:23

Vita na migogoro ya kisiasa inechochea baa la njaa!


Zaidi ya watu millioni moja kutoka Jamhuri ya Watu wa Afrika ya Kati wanakabiliwa na baa la njaa iliyosababishwa kwa kiasi kikubwa na mgogoro wa kisiasa na vita. Taarifa hii imetolewa na Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa, (WFP).

Mauaji ya kinyama, ukosefu wa ulinzi na usalama, ni kati ya mambio yaliyochangia kuzorota kwa uzalishaji mashambani kiasi kwamba, watu wengi wameyakimbia makazi yao na sasa wanakabiliana na baa la naa. Zaidi ya watu elfu mbili walioyakimbia makazi yao hawana uhakika wa usalama wa chakula kwa siku za hivi karibuni.







All the contents on this site are copyrighted ©.