Papa ahimiza, tujikabidhi katika Mkono wa Mungu aliyetuumba
Sote ni lazima tutaipita njia ya kifo. Na ni muhimu kutambua kwamba, katika maisha
haya kuna njia mbili, moja ni njia inayongoonzwa na shetani na njia nyingine ni ile
inayo elekea kwa Mungu. Baba Mtakatifu Francisko ameeleza katika homilia yake, wakati
wa Ibada ya misa mapema Asubuhi, Jumanne hii katika kanisa dogo la Mtakatifu Marta
la hapa Vatican. Papa amesema, Biblia inaelezea kinaga ubaga, juu ya uumbaji
wa Mungu , ambao, kwa mikono yake alituumba sisi sote kutoka matope ya nchi, kwa
sura na mfano wake. Na hivyo kwa mikono yake Mungu alituumba kwa ustadi mkuu. Lakini
sisi binadamu bila kujali tunalisahau hilo na kuitelekeza mikono ya Mungu iliyotuumba,
tukiiacha njia yake na kutembea katika nji aya mwovu shetani. Lakini Mungu aliye
Baba yetu , kama baba na mtoto wake , anaendelea kutufundisha kutembea katika njia
ya maisha inayoongoza katika wokovu. Ni mikono ya Mungu inayo tubembeleza na kuturiwaza
nyakati za mahangaiko na mateso na huzuni kuu za maisha. Kwa mwenye kuishi na Mungu,
huuona upendo huu na Mungu uliojaa neema na faraja kuu. Huwa na baba anayembeleza
kwa upendo mkuu. Papa aliendelea kuasa kwamba kwa bahati mbaya , pamoja na kutubembeleza
na kutuhakikishi ayu pamoja nasi ktika nyakati zote , bado tunamwasi na kumsea kwa
mara nyingi , lakini Yeye hutuvumilia na hachoki kutusamehe. Papa alitoa ushuhuda
wake kwamba, kwake yeye furaha yake na matumaini yake kwamba, daima huguswa na utendaji
wa Yesu ambaye pamoja na kukataliwa na kupambana na mateso makubwa, aliendelea na
mpango wake wa kutuongoza kwa Muungu Baba hadi kifo cha msalabani, kuzikwa na kufufuka
kwa ajili yetu. Na hivyo kwa gharama ya mikono yake iliyo jeruhiwa kwa ajili ya kutupenda
sisi, tunapata mastahili yakuitwa pia watoto wa Mungu. Hii ni faraja kuu.
Papa
Francisko aliendelea kuitafakari Mikono ya Yesu, wakati ikigusa wagonjwa na kuwaponya,
ni mikono hiyohiyo ambayo hata sisi leo hii tukiamini na kulishi neno lake inatuponya
na kutuongoza kwa Mungu. Papa anaona kwa upendo alio nao Mungu kwa binadamu, ni vigumu
kufikiri kwamba Mungu anaweza kumpiga kofi mtu. Mungu ambaye ni upendo daima badala
yake, hutubembeleza na kutufariji wakati wa uchungu na huzuni. Nafsi za wenye haki
ziko katika mikono yake Mungu. Mikono ya Mungu aliye tuumba kwa ustadi, ni hiyohiyo
inayotupa wokovu wa milele, iwapo tutamwamini. . Ni Yeye aliyejuruhiwa mikono anayetuongoza
katika njia hii ya maisha yanayoelekea katika wokovu. Papa alikamilisha homilia
kw kutoa wito kwa kila binadamu, kuona vyema kujikabidhi katika mikono ya Mungu ,
kama mtoto mdogo anavyo jiaminisha katika mikono ya baba yake. Mkono wa Mungu ni Mkono
wa uhakika.