2013-11-12 07:57:06

Baa la njaa laikumba Namibia


Serikali ya Afrika ya Kusini imeamua kushikamana kwa dhati na wananchi wa Namibia katika mapambano dhidi ya baa la njaa linaloendelea kusababisha "majanga" makubwa nchini humo.

Njaa ya mwaka huu haijawahi kutokea nchini Namibia kwa kipindi cha zaidi ya miaka thelathini iliyopita na kwamba, zaidi ya wananchi millioni moja wako hatarini kufa kwa njaa, kama Jumuiya ya Kimataifa haitaonesha mshikamno wa dhati. Idadi hii kwa siku za hivi karibuni imeongezeka na kufikia watu millioni mbili na laki mbili.

Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini baada ya ziara yake ya kikazi nchini Namibia hivi karibuni, ameamua kwamba, Serikali yake itachangia kiasi cha Euro millioni saba na laki mbili. Huu ni mchango wa Serikali ya Afrika ya Kusini katika mapambano dhidi ya baa la njaa na sehemu ya mchakato wa kujenga na kuimarisha ujirani mwema.







All the contents on this site are copyrighted ©.