2013-11-11 09:39:26

Tamko la Familia ya Mungu Tanzania katika kufunga Mwaka wa Imani, Mjini Bagamoyo


Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Jumapili iliyopita, tarehe 10 Novemba 2013 limefunga rasmi Mwaka wa Imani kwa kutoa Tamko la Familia ya Mungu baada ya hija ya kitaifa iliyofanyika mjini Bagamoyo kuanzia tarehe 8 hadi tarehe 10 Novemba 2013. RealAudioMP3

Katika tamko lao, wamefafanua maana, malengo na utekelezaji wa Maadhimisho ya Mwaka wa Imani nchini Tanzania. Makundi mbali mbali yametoa maazimio yanayopaswa kutekelezwa na Familia ya Mungu nchini Tanzania, ili iweze kuwa ni chumvi na mwanga wa dunia. Tamko la Familia ya Mungu nchini Tanzania limesomwa na Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania.







All the contents on this site are copyrighted ©.