2013-11-11 16:27:06

Papa akemea kufadhili Kanisa kwa kuuibia umma.


Papa asema, ni dhambi kubwa kuwa mfadhili wa Kanisa kwa kuiibia serikali. Kufanya hivyo ni kuvaa sura mbili na hivyo ni kuwa kinyume na maisha ya Kikristu.

Papa amekemea wanaotoa msaada Kanisani kwa kutaka waonekanani Wakristu wema kwa kutumia fedha batili. Amesema, hakuna rushwa wala maisha bandia ya kujifanya kuwa Mkristu mwema lakini kumbe ni mtu wa hatari anayeliletea uchungu mkali Kanisa, yanayoweza kusafisha dhambi hiyo ya rushwa. Papa Francisko alieleza wakati wa Ibada ya Misa , mapema asubuhi katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta

Alisema ni kweli sisi sote tuna dhambi, lakini ni lazima kujilinda dhidi ya Rushwa na ulaghai. Na hasa hatari ya kutaka kujionyesha kuwa ni muumini safi , mwenye kutoa msaada kwa kanisa na wahitaji kwa kutumia fedha ya wizi. Kuwaibia wengine, iwe kwa mtu binafsi au serikai au taasisi, na kutumia fdha hiyo kutoa msaada kwa kanisa . Papa anasema kufanya huko si haki, ni sawa na yule anayotoa rushwa ili ahudumiwe, huko ni kuvaa sura mbili katika maisha, ikiwa tofauti na maisha ya Mkristu aminifu.

Papa aliyarejea masomo ya siku ambamo katika Injili, Yesu anatutaka kuwa na moyo wa kusamehe wanao tukosea hata mara saba kwa siku, na kamwe bila kuchoka, inatuonyesha Yeye mwenyewe Yesu asivyochoka kutusamehe pale tunapotubu kwa dhati dhambi zetu.
Wakati Yesu anatutaka kusamehe mara saba kwa siku , alibaini Papa , tunaiona huruma ya Mungu kwa wakosaji.
Lakini pia kifungu hiki cha Injili Yesu anakanya kwa nguvu dhidi ya kuwa watu wachochezi na wazabina zabina na wala rushwa wanaokwaza wengine na kusababisha dhambi.Yesu, alismea, kuliko kumkwaza mmoja wa wadogo hawa, heri mtu huyo afungwwe jiwa la kusagia shingoni na kutupwa baharini. Maneno haya ya Yesu yanatuonyesha jinsi ilivyo vibaya, kuwapotosha watu wengine katika njia za ukweli na aminifu . Papa alieleza na kuhoji, tofauti kati ya dhambi na rushwa.
Papa alifafanua, tofauti ni kwamba mwenye dhambi huyaona makosa yake na kutubu na kuomba msamaha, akijisikia kuwa mnyonge , anajisikia kuwa mtoto wa Mungu, na anajinyenyekesha , na kuomba msamaha kwa Yesu.

Lakini kwa mtoa rushwa ,asiyetaka kutubu badala yake anatoa fedha za wizi kanisani ili aonekane mristu safi, huendelea kuishi katika dhambi ya kujifanya kuwa Mkristo mwema na kumbe anasura nyingine katika maisha ya kawaida yenye kusababisha madhara makubwa na mbaya kwa wengine.
Papa alimwelezea mtu wa aina hiyo , mwenye sura mbili, anapo pambana na vikwazo vya kanisa husema, lakini , mimi ni mfadhili wa Kanisa ! Mimi kwa mkono wangu, natoa zaka na msaada kwa kanisa. Na kumbe kwa upande mwingine, ni mwizi, mwizi anayeibia watu maskini. Haya ni madhulumu makubwa, ambayo Yesu anasema, heri kufungiwa jiwe la kusagia shingoni na kuzamishwa baharini. Hapa Yesu hataji msamaha kwa watu kama haolakini anatoa hukumu.

Hivyo tunaona tofauti za dhambi na rushwa . Papa anaasa kila anaye endesha maisha kwa sura mbili, ni mwovu. Lakini mtu anayetambua makosa yake na kumwendea Bwana kwa unyenyekevu na uchachi na kuomba msamaha kwa Bwana anaye mpenda kw moyo wa dhati, husamehewa, na Bwana huandamana pamoja naye .

Papa ametaja watu wenye maisha ya sura mbili, ni lazima watambue kwamba ni sawa na uzuri wa makaburi yaliyopakaliwa rangi nje lakini ndani yamejaa mifupa ya wafu na uozo. Na Mkristo anayedai kuwa Mkristo, lakini maisha ya si ya Kikristu , ni mtu mwovu, anayetoa rushwa kwa kanisa ili aonekana kwa nje kuwa mtu mwema kumbe sivyo.
Papa alikamilisha homilia yake kwa kumwomba Bwana, neema ya Roho Mtakatifu yenye kuwa na uwezo wa kuufunga uovu na udanganyifu wote, kuomba neema ya kutambua kuwa sisi ni wenye dhambi, na hatutakatifushwi kwa kutoa rushwa , lakini kwa kukutana na Bwana katika sakramenti ya kitubio.








All the contents on this site are copyrighted ©.