2013-11-11 12:13:56

Lugha ya Kilatini bado ni muhimu katika masuala ya Kanisa na Sayansi!


Taasisi ya Lugha ya Kilatini iliyozinduliwa na Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto wa kumi na sita, kunako Novemba 2012, imeendelea kuhamasisha matumizi sahihi ya lugha ya Kilatini kwa kukazia umuhimu wa lugha hii kwa watu mbali mbali. Kuna baadhi ya watu wanaendelea kudhani kwamba, Kilatini ni lugha ambayo imepitwa na wakati, lakini ukweli wa mambo unaonesha kwamba, Kilatini bado kinaendelea kutumika na kwamba, hii ni lugha ya Kanisa na Wasomi kutoka katika medani mbali mbali zamaisha kama alivyobainisha Professa Ivano Dionigi, Rais wa Taasisi ya Kipapa ya Lugha ya Kilatini wakati wa kuzindua Jarida Jipya lijulikanalo kama "Latinitas".

Makala ya kwanza inajikita zaidi na zaidi katika mchango ambao umetolwa na Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto wa kumi na sita katika kufufua na kukuza lugha ya Kilatini. Jarida hili limegawanyika katika sehemu kuu tatu: sehemu ya kwanza inajihusisha na masuala ya kisayansi; sehemu ya pili inajikita katika masuala ya Fasihi Simulizi na Ufundishaji wa lugha na tamaduni za kale.

Uzinduzi wa Jarida hili umehudhuriwa na viongozi wakuu kutoka Vatican na kati yao alikuwa ni Kardinali Gianfranco Ravasi, Rais wa Baraza la Kipapa la Utamaduni.







All the contents on this site are copyrighted ©.