Kifo kiko nyuma yetu,na mbele yetu kuna Mungu wa walio hai- Papa
Baba Mtakatifu Francisko, kabla ya kusali sala ya Malaika wa Bwana, mbele ya mahujaji
na wageni waliokusanyika katika Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, Vatican,
alitoa hotuba fupi, akilenga zaidi somo la Injili la Jumapili , ambapo Yesu alikabiliana
na Masadukayo , ambao hawakusadiki juu ya ufufuko wa wafu.
Francisko
alisema,Masadukayo waliitoa swali hili la mwanamke kuolewa na ndugu saba , kwa makusudi
ya kumtega na kukejeri ufahamu wa Yesu juu ya Imani katika ufufuo. Masadukayo walihoji
sasa mke huyo aliyeolewa na wamanume saba, ambao walikufa mmoja baada ya mwingine,
je wakati wa ufufuo , nani atakuwa mme wa mwanamke huyo ? Awali ya yote,
Papa alisema , Yesu anaeleza kwamba maisha baada ya kifo ni maisha mengine tofauti
na maisha yetu ya duniani. Uzima wa milele ni maisha tofauti, yenye mwelekeo tofauti
ambapo , miongoni mwa mambo mengine, hapatakuwepo tena maisha ya ndoa. Kufufuka,
Yesu anasema, ni kuwa mwili mwingine kama malaika , na wao wataishi katika hali mbalimbali,
ambazo sisi hapa duniani hatuwezi kuziishi wala hatuna sura yake inavyo fanana hatunayo
hata kimwazo tu.
Lakini basi, Papa Francisko aliendelea , Yesu anatoa
majibu na kuzungumzia suala hili, na kutoa mfano wa tukio la Musa na kijiti cha moto,
ambapo Mungu alijifunua mwenyewe kuwa ni Mungu wa Abrahamu, Isaka na Yakobo. Jina
la Mungu , Papa Francis alielezea, linatufugamanisha na majina ya wanaume na wanawake
ambao Yeye ana mahusiano nao. Ni kiungo chenye nguvu, kuliko kifo. Hii ndiyo sababu
Yesu anasema kwa uthabiti kwamba, Yeye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai kwa wote
walioitwa kuishi kwake (Luka 20:38 ). Yesu ndiye kiungo muhimu,Yeye aliye Uzima na
Ufufuo , kwa sababu kwa upendo wake alikubali kusulubiwa na kukishinda kifo .
Katika
Yesu , Papa alisema, Mungu anatupa uzima wa milele : Yeye anautoa kwa kila mtu. Shukrani
kwakeYeye anayetupa tumaini hili, maisha tumaini lililo kuu kuliko yote. Maisha
ambayo Mungu ametuhifadhia ghalani mwake si tu kwa ajili ya maisha bora zaidi lakini
ni imaisha ambayo akili yetu ya kibinadamu, haiwezi kufikia upeo wake, kwa sababu
Mungu daima , hutushangaza kwa upendo na huruma yake.
Kwa hiyo, Francis
Papa alielezea, kitakachotokea ni kinyume kabisa na kile Masadukayo walivyotarajia.
Maisha ya hapa duiniani hayawezi kuwa kiwango cha maisha ya milele : ni umilele, ulio
kinyume na maisha yetu , ni umilele wenye kuangazia maisha ya hapa duniani na kutoa
tumaini kwetu. Iwapo tutatazama kwa macho ya kibinadamu , Papa aliendelea , tunakuwa
na mwelekeo wa kuona kwamba, njia ya maisha tunayo itembea inaelekea katika kifo.
Lakini Yesu anatutazamisha katika lengo kuu la Maisha, akituthibitishia kwamba tunatembea
katika safari inayokwenda kutoka kifo kuelekea maisha kamili ya umilele. Hivyo
, Papa alihitimisha hotuba yake na maelezo kwamba kifo kiko nyuma yetu, si mbele
yetu . Mbele yetu ni Mungu wa walio hai, aliyeshinda hila zote za kifo na dhambi
na mauti, na kuwa mwanzo wa maisha mpya ya furaha na mwanga na usio na ukomo. Lakini
tayari katika dunia hii - katika sala, katika Sakramenti , katika udugu - sisi kukutana
Yesu na upendo wake, na ili tuweze kupata ladha ndogo ya maisha ya kufufuka.