2013-11-09 14:39:54

Hija za maisha ya kiroho, ziwawezeshe waamini kuwa karibu na Kristo, ili kumshirikisha shida na mahangaiko yao ya ndani!


Baba Mtakatifu Francisko amewashukuru waamini na viongozi wa Kanisa kutoka Liguria, kwa ari, moyo, upendo na mshikamano wa dhati wanaouonesha kwa Khalifa wa Mtakatifu Petro. Anasema, kila mwamini anayefanya hija ya maisha ya kiroho mjini Vatican anayo nia maalum moyoni mwake anayopenda kumshirikisha Yesu.

Huu ni muda muafaka wa kuweza kujenga na kudumisha uhusiano wa karibu na Kristo kwa njia ya sala, kwani Yesu daima anawangoja ili kuwakaribisha na kuwapokea, ili aweze kuwaonjesha huruma na upendo wake usiokuwa na kikomo! Kristo yuko tayari kuwasikiliza na kuwatimizia shida na mahangaiko yao kadiri ya mpango wake.

Amewaomba mahujaji kutoka Liguria, nchini Italia kuwafikishia salam na matashi mema ndugu na jamaa zao waliobaki nyumbani. Kwa mara nyingine tena, Baba Mtakatifu Francisko amewaomba waamini kusali kwa ajili yake.







All the contents on this site are copyrighted ©.