Rais Laura Nchinchilla wa Costa Rica akutana na kuzungumza na Papa Francisko
Baba Mtakatifu Francisko, Ijumaa tarehe 8 Novemba 2013 amekutana na kuzungumza na
Rais Laura Nchinchilla kutoka Costa Rica ambaye baadaye pia alikutana na kuzungumza
na Askofu mkuu Dominique Mamberti, Katibu mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano
wa kimataifa mjini Vatican.
Viongozi hawa wawili wamefurahisha na uhusiano
mzuri uliopo kati ya Kanisa na Serikali na kwamba, wamekuwa wakishirikiana kwa pamoja
katika kutafuta ufumbuzi wa masuala kadhaa yanayowakabili wananchi wa Costa Rica.
Kwa pamoja wameendelea kusimama kidete kulinda na kutetea zawadi ya uhai na utunzaji
bora wa mazingira.
Kimsingi viongozi hawa wawili wamekubaliana kuanzisha mchakato
utakaoimarisha uhusiano wa karibu zaidi kati ya Vatican na Costa Rica kwa ajili ya
mafao na maendeleo ya pande hizi mbili. Baba Mtakatifu pamoja na mgeni wake wamegusia
pia masuala ya kikanda na kimataifa kwa kutilia mkazo umuhimu wa ujenzi wa amani.